MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali Yaitaka TBS Kuongeza Ubunifu, Usasa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali Yaitaka TBS Kuongeza Ubunifu, Usasa
Habari

Serikali Yaitaka TBS Kuongeza Ubunifu, Usasa

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Na Lucy Ngowi

DODOMA: WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amelielekeza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuharakisha matumizi ya teknolojia za kisasa, kujitegemea kifedha na kuongeza utoaji wa elimu kwa umma ili kuimarisha ubora wa bidhaa, kurahisisha biashara na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

Kapinga ametoa maelekezo hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya TBS, akisema shirika hilo lina nafasi muhimu katika kufanikisha azma ya Tanzania ya kujenga uchumi wa viwanda wenye ushindani katika soko la ndani na kimataifa.

Amesema baada ya kufikisha miaka 50, TBS inapaswa kuanza kujitegemea zaidi kifedha badala ya kuendelea kutegemea ruzuku kutoka Serikalini.

Habari Picha 12474

“Miaka 50 ni umri wa taasisi iliyokomaa. Ni wakati wa TBS kujitegemea na kuondoa mzigo kwa mfuko mkuu wa Serikali huku ikichangia zaidi maendeleo ya taifa,” amesema.

Waziri huyo pia amesisitiza umuhimu wa kuboresha mifumo ya kidijitali na kuunganisha huduma za TBS na taasisi nyingine ili kupunguza vikwazo vya biashara, hususan katika maeneo ya mipakani.

Amesema dunia imebadilika na kwamba wananchi wanapaswa kuwa na uwezo wa kuthibitisha ubora wa bidhaa kwa kutumia teknolojia za kisasa kama mifumo ya kielektroniki inayoweza kusomwa kwa njia ya simu.

Kapinga ameongeza kuwa TBS ina jukumu kubwa la kulinda afya ya jamii kupitia udhibiti wa ubora wa vyakula na vipodozi, hivyo ni muhimu kuanzisha programu endelevu za kutoa elimu kwa wananchi kuhusu viwango vinavyotakiwa kufuatwa katika bidhaa mbalimbali.

Aidha, amewataka watendaji wa shirika hilo kujiona kama wawezeshaji wa biashara na viwanda badala ya kuwa kikwazo kwa wawekezaji na wafanyabiashara.

Akizungumzia mafanikio ya TBS katika kipindi cha miaka 50, Kapinga amesema yamechangiwa na maono ya viongozi waliopita, juhudi za wafanyakazi pamoja na ushirikiano wa wadau mbalimbali.

Ameeleza matarajio ya Serikali kuwa katika miaka 50 ijayo, TBS itaendelea kuwa taasisi ya kisasa, bunifu na yenye uwezo mkubwa wa kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia, biashara na mahitaji ya soko la dunia.

You Might Also Like

CHAKUHAWATA Yaimarisha Ulinzi wa Haki za Walimu, Yafikia Wanachama 49,750

Theluthi mbili ya nguvu kazi ya taifa ipo kwenye kilimo

DC Twange Apongeza Wananchi Kuchangia Maendeleo 

Chagueni Viongozi Wanaofaa-Biteko

Mabalozi Wa Utalii Waahidi Kuulinda Ushoroba Wa Kwakuchinja

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TBA Yaongeza Elimu kwa Wananchi Kuhusu Huduma na Miradi ya Uwekezaji
Next Article PSSSF Yafanya Maisha Kuwa Rahisi Kwa Wanachama
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

PSSSF Yafanya Maisha Kuwa Rahisi Kwa Wanachama
Habari June 20, 2026
TBA Yaongeza Elimu kwa Wananchi Kuhusu Huduma na Miradi ya Uwekezaji
Habari June 19, 2026
WRRB YATOA FURSA MPYA KWA WAFUGAJI NCHINI
Habari June 19, 2026
Mfumo Wa  PPAA Waongeza Ufanisi  Kusimamia Malalamiko Ya Zabuni
Habari June 19, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?