MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: PSSSF Yafanya Maisha Kuwa Rahisi Kwa Wanachama
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > PSSSF Yafanya Maisha Kuwa Rahisi Kwa Wanachama
Habari

PSSSF Yafanya Maisha Kuwa Rahisi Kwa Wanachama

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Lucy Lyatuu,Dodoma

MABORESHO yaliyofanywa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kupata huduma kupitia PSSSF Kidijitali yameleta urahisi kwa wanachama wa Mfuko hu.

Hayo yamebainishwa na wanachama wa Mfuko waliotembelea kwenye banda la PSSSF kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Ofisa Utumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TARIRI), Odilia Marenga amebainisha alipotembelea banda la huduma la PSSSF katika viwanja hivyo kuwa watumishi wa TARIRI walionufaika na mafao kutoka PSSSF ni shuhuda, wamekuwa wakipiga simu kueleza furaha yao kwa jinsi walivyopokea mafao haraka.

Habari Picha 12480

“Tangu huduma zianze kutolewa kupitia PSSSF portal, zimekuwa zikitolewa kwa wakati, tofauti na hapo nyuma… hali hii imekuwa ikiwafurahisha wastaafu wetu na wale akina mama wanaoomba fao la uzazi,” amesema Marenga.

Kwa upande wake Mwanachama wabPSSSF Rebeca Hoza, amesifu huduma ya PSSSF Kidijitali, ambayo amekuwa akipata huduma kupitia kiganjani.

“Nikitaka kuangalia michango yangu au taarifa zozote, sihangaiki tena, PSSSF wamefanya maisha yetu kuwa rahisi.” amesema.

Kuhusu mafanikio ya utoaji huduma, Kaimu Meneja wa PSSSF Kanda ya Kati- Dodoma, Jane Mbuya amewashukuru wanachama wa PSSSF kwa kuonyesha ushirikiano kwa kutumia huduma hiyo ya PSSSF portal.

Habari Picha 12481

“Ushuhuda ni kwamba hata ukipita kwenye ofisi zetu hutakuta foleni za wanachama wakipata huduma, kwani tumesogeza huduma kupitia PSSSF Kidijitali hii imeturahisishia, sasa hivi tunachakata mafao ya mstaafu kabla hajaondoka ofisini, akistaafu na mafao yake yako tayari, hii ni kutokana na kutumia mifumo kutoa huduma,” amesisitiza Mbuya.

Habari Picha 12482

You Might Also Like

BoT Yarahisisha Uuzaji wa Dhahabu kwa Wachimbaji, Yatoa Punguzo La Mrabaha

Wanaosimamia Mitandao Ya Serikali Wadhibiti Usalama Wake

Serikali  Kuja Na Mradi  Wa Kuimarisha Upatikanaji Umeme Vitongojini- Kapinga 

Wastaafu Watakiwa Kutafuta Ushauri  Wa Kitaalam Kwa Matumizi Ya Mafao

‎NIRC Imechimba Visima 362, , Yahamasiha Wakulima Kunufaika Na Program Ya Umwagiliaji

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Yaitaka TBS Kuongeza Ubunifu, Usasa
Next Article
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mfumo Wa Kidijitali Wa PSSSF Wamvutia Mkurugenzi Wa BOT
Habari August 5, 2026
FAO Yasisitiza Kutowapa Mifugo Dawa Bila Maelekezo Ya Watalaam
Habari August 5, 2026
Balozi Wa Kudumu Wa Mashirika Ya UN Atembelea FAO Nanenane
Habari August 5, 2026
Wadau Wamiminika Banda La REA Katika Maonesho Ya Nanenane  2026
Habari August 5, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?