MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: FAO Yasisitiza Kutowapa Mifugo Dawa Bila Maelekezo Ya Watalaam
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > FAO Yasisitiza Kutowapa Mifugo Dawa Bila Maelekezo Ya Watalaam
Habari

FAO Yasisitiza Kutowapa Mifugo Dawa Bila Maelekezo Ya Watalaam

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Lucy Lyatuu, Dodoma

SHIRIKA la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) linasisitiza umuhimu wa kutumia dawa kwa ajili ya mifugo pale inapobidi na kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu au chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya ya mifugo.

Ujumbe huo umetolewa na Mratibu Wa Miradi Ya Udhibiti Wa Usugu Wa Vimelea Vya Magonjwa Dhidi Ya Dawa kutoka FAO, Elibariki Mwakapeje, wakati akizungumza katila maonesho ya Nanenane yanayoendelea Dodoma.

Habari Picha 13120

Amesema elimu hiyo inalenga kuwajengea wafugaji uelewa kuhusu matumizi sahihi na yenye uwajibikaji ya dawa za mifugo, pamoja na madhara yanayoweza kujitokeza endapo dawa zitatumika bila kuzingatia ushauri wa wataalamu.

Amesema wanatumia Maonesho ya Nane Nane kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu namna ya kukabiliana na usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa, hali inayoweza kupunguza ufanisi wa dawa za kutibu na kudhibiti magonjwa kwa mifugo.

Mwakapeje amesema wafugaji wanapaswa kuepuka kutibu mifugo bila ushauri wa wataalamu wa afya ya mifugo, huku akisisitiza umuhimu wa kutumia dawa pale inapobidi na kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu au chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya ya mifugo.

Habari Picha 13121

Ameongeza kuwa wafugaji wanapaswa pia kuzingatia usafi wa mazingira, mabanda, vyombo vya maji na chakula cha mifugo, hatua inayosaidia kuzuia na kupunguza maambukizi ya magonjwa na hivyo kupunguza utegemezi usio wa lazima wa dawa katika kutibu mifugo.

Kwa mujibu wa Mwakapeje, matumizi holela ya dawa yanaweza kuongeza usugu wa vimelea vya magonjwa, jambo linaloweza kuathiri afya ya mifugo, wanyama wengine, binadamu na usalama wa chakula.

Amesema suala hilo linahitaji ushirikiano wa wafugaji, wataalamu wa afya ya mifugo na wadau wengine katika mnyororo wa chakula ili kuhakikisha dawa zinatumika kwa usahihi.

Amesema FAO itaendelea kutumia majukwaa kama Maonesho ya Nane Nane kuwaelimisha wananchi kuhusu matumizi salama na yenye uwajibikaji ya dawa, akisisitiza ujumbe wa “Kinga ni bora kuliko tiba” katika mapambano dhidi ya usugu wa vimelea vya magonjwa na kulinda afya ya mifugo pamoja na usalama wa chakula.

You Might Also Like

Taasisi za Elimu Geita Zatakiwa Kuanza Programu ya Maziwa Shuleni

Ndege Ya TPHPA Yatua Rasmi Kudhibiti, Kwelea Kwelea, Viwavijeshi, Nzige 

WCF Yatakiwa Kuongeza Nguvu Kusajili Waajiri

Profesa Nombo Azindua Miongozo Ya Usimamizi Ya Utafiti, Ubunifu COSTECH

Watahiniwa 72 wa kidato cha nne wafutiwa mtihani kwa udanganyifu, kuandika lugha za matusi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Balozi Wa Kudumu Wa Mashirika Ya UN Atembelea FAO Nanenane
Next Article Mfumo Wa Kidijitali Wa PSSSF Wamvutia Mkurugenzi Wa BOT
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mfumo Wa Kidijitali Wa PSSSF Wamvutia Mkurugenzi Wa BOT
Habari August 5, 2026
Balozi Wa Kudumu Wa Mashirika Ya UN Atembelea FAO Nanenane
Habari August 5, 2026
Wadau Wamiminika Banda La REA Katika Maonesho Ya Nanenane  2026
Habari August 5, 2026
FAO Yatoa Mafunzo Kwa Wadau Wa Uvuvi Kutumia Teknolojia Zinazoboresha Uzalishaji Mazao Ya Uvuvi
Habari August 5, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?