MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Magereza Yaomba Jamii Kuwapokea Wafungwa Wanaorejea Kutumikia Taifa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Magereza Yaomba Jamii Kuwapokea Wafungwa Wanaorejea Kutumikia Taifa
Habari

Magereza Yaomba Jamii Kuwapokea Wafungwa Wanaorejea Kutumikia Taifa

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Na Lucy Ngowi

DODOMA: JESHI la Magereza limewataka wananchi kubadili mtazamo dhidi ya wafungwa wanaomaliza vifungo vyao kwa kuwapa fursa ya kuanza maisha mapya, likieleza kuwa mfumo wa kisasa wa magereza unalenga zaidi marekebisho ya tabia na kuwaandaa wahusika kuwa raia wema baada ya kutumikia adhabu zao.

Akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Elmas Mgimwa, amesema taasisi hiyo imeimarisha programu za marekebisho zinazowajengea wafungwa ujuzi na stadi mbalimbali za maisha ili waweze kujitegemea wanaporejea katika jamii.

Habari Picha 12427

Amesema mbali na jukumu la msingi la kupokea na kuhifadhi wafungwa kwa mujibu wa sheria, magereza yanaendesha mafunzo ya ufundi stadi, kilimo, ujasiriamali na elimu nyingine zinazowawezesha wafungwa kupata maarifa yatakayowasaidia kujenga maisha yao baada ya kifungo.

“Tunataka kila anayemaliza kifungo atoke akiwa amepata mabadiliko chanya, maarifa na ujuzi wa kujitegemea ili aweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya familia yake na taifa kwa ujumla,” amesema Mgimwa.

Amefafanua kuwa mchakato wa marekebisho huanza tangu mfungwa anapopokelewa gerezani, kupitia programu za kujenga maadili na tabia njema, hadi hatua ya kuandaliwa kurejea katika jamii.

Habari Picha 12428

Mgimwa amesisitiza umuhimu wa wananchi kuwaunga mkono waliomaliza vifungo badala ya kuwabagua, akieleza kuwa lengo la kifungo ni kutoa nafasi ya marekebisho kama ambavyo mgonjwa hupatiwa matibabu ili kurejea katika hali bora.

Aidha, amesema Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na maandalizi ya kuanzisha mfuko maalumu utakaowawezesha wafungwa wanaomaliza vifungo kuanzisha shughuli za kiuchumi kulingana na stadi walizopata wakiwa magerezani.

Kwa mujibu wa Mgimwa, hatua hiyo itachangia kupunguza matukio ya wahusika kurejea katika makosa ya jinai na badala yake kuwa sehemu ya nguvu kazi inayochochea maendeleo ya nchi.Pia, Jeshi la Magereza linaendelea kufuatilia maendeleo ya waliomaliza vifungo ili kuhakikisha wanatumia vyema elimu na ujuzi walioupata wakati wa kutumikia adhabu zao.

You Might Also Like

July 10, 2025

Profesa Kabudi Atoa Maagizo Mazito Bodi Ya Ithibati Ya Waandishi Wa Habari

Kisima Kimoja Cha Gesi Chaonesha Mshangao Kwa Uzalishaji Wa Gesi-PURA

Serikali Kuja Na Mwongozo Wa Kuimarisha Ushirikishwaji Jamii Katika Masuala Ya Afya

Naibu Waziri Katambi Asisitiza Ufanisi na Ubunifu Kwenye SIDO

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TPHPA Yasisitiza Matumizi Sahihi ya Viuatilifu kwa Wakulima
Next Article
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Hananja Awataka Vijana Kufikiri Mara Mbili Kabla ya Kufuata Wito wa Maandamano
Habari June 18, 2026
June 18, 2026
Habari June 18, 2026
TPHPA Yasisitiza Matumizi Sahihi ya Viuatilifu kwa Wakulima
Habari June 18, 2026
BRELA Yahamasisha Urasimishaji wa Biashara kwa Ukuaji wa Uchumi
Habari June 18, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?