MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TPDC Kufikisha Gesi Nchi Nzima  Ndani Ya Miaka Miwili Na Nusu  Kuanzia Sasa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TPDC Kufikisha Gesi Nchi Nzima  Ndani Ya Miaka Miwili Na Nusu  Kuanzia Sasa
Habari

TPDC Kufikisha Gesi Nchi Nzima  Ndani Ya Miaka Miwili Na Nusu  Kuanzia Sasa

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na  Lucy Lyatuu,Dodoma
SHIRIKA La Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) limesema lina mpango wa kusogeza huduma ya vituo vya kusambaza gesi nchi nzima na kwamba ndani ya miaka miwili na nusu  kuanzia sasa huduma hiyo itafikishwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mussa Makame amesema hayo  wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kutangaza miradi ya maendeleo na fursa za vijana kwa mwaka 2025/2026.
 Amesema TPDC inahimiza ujio wa vijana kwenye sekta ya nishati, ambapo asilimia 79 ya wafanyakazi ni vijana.
Kuhusu kusogeza huduma ya vituo vya CMF  amesema kwa sasa Tanzania Ina vituo 14 peke yake na vimejengwa katika mkoa wa Dar es Salaam na Kwa kuanzia huduma hiyo itasogezwa katika vituo vidogo katika mkoa ya Tanga,Kilimanjaro,Arusha,Dodoma na Morogoro ambapo vitafikisha gesi kama ilivyo bila kuchakatwa.
Amesema kwa maneno mengine Kwa kushirikiana na  kampuni mbalimbali  gesi itafikishwa kwa mfumo wa LNG yaaani kubadilisha gesi kuwa kimiminika  ambapo itafikishwa nchi nzima ndani ya kipindi hicho.
Aidha amesema nyumba 2500 kutoka mikoa ya Mtwara,Lindi na Dar es Salaam zitaunganishwa Kwa gesi.
Ameongeza kuwa TPDC inaendelea kuchangia maendeleo ya Taifa kwa kuendesha miradi mikubwa ya nishati, huku ikiweka kipaumbele katika kuwajengea uwezo vijana wa Kitanzania.
Almesema katika mwaka wa fedha 2025/2026, TPDC inaendelea kutekeleza miradi kwa Awamu , inayolenga kuongeza upatikanaji wa gesi asilia, kupanua usambazaji wa mafuta na gesi, na kutoa fursa kwa vijana kuajiriwa, kupata mafunzo na kushiriki katika mnyororo wa thamani wa sekta ya nishati.
Amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho za majadiliano ya mradi wa gesi asilia wa kimkakati unaogharimu Dola bilioni 42 na kwamba TPDC inahakikisha ushiriki wa vijana na wazawa katika ajira, ujenzi, zabuni, huduma za kitaalamu, TEHAMA, na malazi.
Ameitaja  miradi mikuu inayotekelezwa na Shirika hilo ni pamoja na Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), ambapo ujenzi wa bomba kutoka Hoima, Uganda hadi Bandari ya Tanga umefikia asilimia 81 na unatarajiwa kukamilika Julai mwaka huu na kwamba mradi huo  unatoa ajira,fursa za zabuni na uhamasishaji wa ujuzi kwa Watanzania.
“Fursa zinazotolewa ni ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, mafunzo ya vitendo, zabuni, “internship programs” na uwezeshaji wa sekta za kiuchumi kama usafirishaji, viwanda na hoteli,” amesema.
Kuhusu miradi ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), ameeleza kuwa
zaidi ya Sh bilioni 11.5 zimegawanywa kwenye miradi ya kijamii ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya, shule, kivuko, taa za barabarani, na kituo cha polisi.
Akizungumzia uchorongaji wa visima vitatu Mnazibay, Mtwara ameeleza kuwa Kisima cha kwanza (MB-5) kimeanza Februari mwaka huu  na miradi yote itakamilika Oktoba 2026.
Makame Akizungumzia utafutaji wa mafuta Kitalu cha Eyasi Wembere amebainisha kuwa TPDC inaendelea na uchukuaji wa taarifa za 2D katika mikoa ya Singida, Tabora, Simiyu, Arusha na Shinyanga, ukikamilika Juni 2027 kwa gharama ya Shilingi bilioni 53.4.

You Might Also Like

Waziri Mkuu Mstaafu Pinda Atoa Neno Kwa Vijana, Maadhimisho Miaka 30 VETA

TUCASA Yatoa Mapendekezo ya Sheria, Sera Kwa Serikali Kutatua Ucheleweshaji Wa Malipo

Serikali Kuimarisha Uvuvi Bahari Kuu Kupitia TAFICO

TFRA yazindua Chama cha wafanyabiashara wa Mbolea

Vita Mashariki ya Kati Vyatikisa Uchumi wa SADC, Mawaziri Watakiwa Kuchukua Hatua

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Nchimbi Ahimiza Ushirikiano wa Wizara Katika Uhifadhi wa Mazingira
Next Article GCLA  Yanunua Mitambo Mikubwa Inayogharimu Sh Bil 32.25 Kuimarisha Uchunguzi Wa Sampuli
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Serikali Yaingia Makubaliano Ya Ushirikiano Na DIT Kuimarisha Usimamizi Wa Mataifa
Habari June 8, 2026
Wananchi Waelimishwa Masharti ya Kubadilisha Noti Zilizochakaa, Kuungua na Kuchanika
Habari June 7, 2026
DMI Yawaalika Vijana Kujiunga Na Masomo Ya Ubaharia
Habari June 6, 2026
Taifa Gas Yaendelea Kuongoza Kampeni ya Nishati Safi kwa Taasisi na Sekta ya Utalii Tanzania
Habari June 6, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?