MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TUCTA: Waajiri Watekeeze Nyongeza Ya Kima cha Mishahara Sekta Binafsi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TUCTA: Waajiri Watekeeze Nyongeza Ya Kima cha Mishahara Sekta Binafsi
Habari

TUCTA: Waajiri Watekeeze Nyongeza Ya Kima cha Mishahara Sekta Binafsi

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
NJOMBE: RAIS wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya, amewataka waajiri nchini kutekeleza amri ya nyongeza ya Kima cha Chini cha mishahara kwa wafanyakazi wa sekta binafsi kama inavyofanywa na Serikali.
Nyamhokya ametoa kauli hiyo leo Aprili 27, 2026 alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano katika maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yanayoendelea mkoani Njombe.
Alisema Serikali ilitangaza kima hicho cha chini cha mishahara ambacho kimeanza kutumika mwezi Januari mwaka huu 2026, ambapo hadi sasa takwimu zinaonesha ni takribani asilimia 80 tu ya waajiri katika sekta binafsi wameanza kutekeleza.
Habari Picha 11915
“Nitoe wito kwa waajiri wa sekta binafsi nchini kutekeleza amri hii ya serikali kwa kuongeza mishahara husika… hatua itakayochangia ustawi na morali ya wafanyakazi,” alisisitiza Rais huyo wa TUCTA.
Akiwa katika banda hilo, Nyamhokya alipokea maelezo ya elimu zinazotolewa, ikiwemo elimu ya huduma za ajira, kinga ya jamii, sheria za kazi nchini pamoja na mahusiano baina ya Serikali na Makundi ya Kijamii yanayo jumuisha Taasisi za Dini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali,Wadau wa Siasa na Asasi za kiraia.
Alipongeza maofisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa elimu wanayoitoa kwa umma kwenye maonesho hayo, akisema inaakisi huduma za wizara kwa wananchi na wafanyakazi.
Pia, Nyamhokya amewaasa wananchi na wafanyakazi kuendelea kutembelea banda hilo ili kupata elimu zaidi ikiwemo elimu ya kinga ya jamii.
Katika hatua nyingine, Rais wa TUCTA amewasihi wafanyakazi mkoani Njombe na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi katika sherehe za Mei Mosi zinazotarajiwa kufanyika kitaifa katika mkoa huo.

You Might Also Like

Balozi Seokolo Atoa Wito Kuimarisha Biashara na Viwanda Kanda ya SADC

Serikali Yaja Na Kanuni Mpya Ya Sheria Ya Fidia   Kuboresha Mazingira Ya Mfanyakazi 

Mnyororo wa Biashara Kariakoo Unafanywa Na Wageni

Waziri Mkuu Majaliwa Azungumzia Urushaji Wa Satelite Tanzania

Waomba Kuondolewa Vikwazo Vya Biashara Ya Mazao Ya Kilimo Ikolojia Mipakani

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Yaweka Mkazo Kufufua Viwanda Musoma Ili Kuongeza Ajira
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Serikali Yaweka Mkazo Kufufua Viwanda Musoma Ili Kuongeza Ajira
Habari April 24, 2026
Program Ya Mama Samia Ya Kurasimisha Ujuzi Yazinduliwa
Habari April 23, 2026
TEA, Wizara ya Elimu Zanzibar Kushirikiana Kuimarisha Miradi ya Elimu
Habari April 23, 2026
Bajeti Yadhihirisha Uhakika Wa Nishati Nchini
Habari April 23, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?