MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Rais Samia ashuhudia JOWUTA Ikiwa mwanachama wa  TUCTA 
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Rais Samia ashuhudia JOWUTA Ikiwa mwanachama wa  TUCTA 
Habari

Rais Samia ashuhudia JOWUTA Ikiwa mwanachama wa  TUCTA 

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Lyatuu, Singida
CHAMA cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA),  kimetangazwa rasmi kuwa mwanachama wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA).
Taarifa hiyo ya kufurahisha kwa JOWUTA imetolewa na Katibu Mkuu wa TUCTA, Henry Nkunda, wakati  akisoma risala ya wafanyakazi mbele ya Rais Samia, kwenye maadhimisho ya sherehe za Mei mosi Kitaifa zilizofanyika kwenye Viwanja vya Bombadia mjini Singida leo.
Nkunda amesema pamoja na JOWUTA vyama vingine ambavyo vilivyopokelewa kama wanachama wapya ni Chama cha Wafanyakazi wa Kampuni Binafsi za Ulinzi nchini (TUPSE) na Chama cha Wafanyakazi za Huduma za Viwandani Tanzania (TASIWU).
Baada ya vyama hivyo vitatu kuwa mwanachama rasmi wa TUCTA sasa itakuwa na jumla ya vyama vya wafanyakazi  wanachama 16.
“Mheshimiwa Rais TUCTA ilipokea maombi ya vyama tisa vya wafanyakazi ambapo baada ya Bazara Kuu kukutana na kujadili vyama vitatu vya JOWUTA, TUPSE na TASIWU vimefanikiwa kukidhi vigezo na kujiunga na shirikisho hili, bado tunaendelea na mchakato wa kuunga vyama vingine , lengo letu ni kuwa wamoja,” amesema.
Akizungumza mjini hapa na viongozi wa JOWUTA ,Rais wa TUCTA Tumaini Nyamuhokya amepongeza JOWUTA na vyama vingine kudumisha ushirikiano na kufanya kazi na shirikisho kwa maslahi ya wanachama.
“Mimi muda mrefu nilikuwa napenda JOWUTA mkamilishe taratibu na kuwa wanachama wa TUCTA ili tusaidiane kusaidia tasnia yenu”amesema
Mwenyekiti wa Taifa wa JOWUTA, Mussa Juma amemweleza Rais huyo wa TUCTA kuwa JOWUTA imepokea kwa furaha kubwa tangazo la kukubaliwa kuwa mwanachama wa shirikisho.
Amesema JOWUTA itajitahidi kufuata taratibu na Kanuni za TUCTA, ili kuwa mwanachama hai na hivyo kushirikiana kutatua changamoto katika tasnia ya habari nchini.
“Tunashuru sana kukubaliwa maombi yetu ya muda mrefu kuwa mwanachama wa TUCTA na sasa tunaimani kwa kutumia uzoefu wa TUCTA katika kushughulika na masuala ya kazi, ili wafanyakazi wa vyombo vya habari wanufaike”amesema
Naye Katibu wa JOWUTA Selemani Msuya amesema chama hicho kukubaliwa kujiunga  TUCTA ni ushahidi tosha kwamba linapambania maslahi ya wanachama wake na kuwataka wanachama wake walipe ada kwa wakati ili kujenga ushirikiano huo.
“Hii ni habari njema kwetu sisi JOWUTA, napenda kutumia nafasi hii kuwaomba wanachama walipe ada kwa wakati na waandishi wengine wajiunge ili kuwa na nguvu pamoja katika kupigania maslahi yetu,” amesema.

You Might Also Like

Kiwanda cha Sukari Mkulazi Chaanza Kuleta Tija, Sangu Apongeza Uwekezaji wa NSSF na Magereza

Brela Yatoa Huduma Zote Za Usajili Katika Maonesho Ya Teknolojia Ya Madini Geita

CMA Inasaidia Vijana Kuwa Na Nafasi Bora Kazini

Wataalam wa “Visit Finland” Wabadilishana Uzoefu Kutangaza Utalii Duniani 

Hotuba ya Rais Samia Yachochea Miradi Mikubwa ya Viwanda na Bandari Bagamoyo – Mgalu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TEA Mshindi wa Kwanza Maonyesho Ya Mfuko wa Utamaduni
Next Article Kima Cha Chini Cha Mshahara Chapanda Kwa Asilimia 35.1-Rais Samia
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TBA Yaongeza Elimu kwa Wananchi Kuhusu Huduma na Miradi ya Uwekezaji
Habari June 19, 2026
WRRB YATOA FURSA MPYA KWA WAFUGAJI NCHINI
Habari June 19, 2026
Mfumo Wa  PPAA Waongeza Ufanisi  Kusimamia Malalamiko Ya Zabuni
Habari June 19, 2026
TBA Yakaribisha Wawekezaji Kushirikiana  Kwenye  Miradi Ya Ujenzi
Habari June 19, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?