MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: NSSF Yafikia Trilioni 11.2, Hifadhi Skimu Yatajwa Kubadili Maisha ya Watanzania
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > NSSF Yafikia Trilioni 11.2, Hifadhi Skimu Yatajwa Kubadili Maisha ya Watanzania
Habari

NSSF Yafikia Trilioni 11.2, Hifadhi Skimu Yatajwa Kubadili Maisha ya Watanzania

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu,

DODOMA: MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeendelea kuimarika kwa kasi, ukifikia thamani ya Sh Trilioni 11.2 hadi Machi 2026 kutoka Trilioni 4.3 mwaka 2020, hatua inayoonesha ukuaji wa uwekezaji, uimara wa usimamizi na ongezeko la wanachama kupitia Hifadhi Skimu.

Akizungumza jijini Dodoma April 27, 2026 wakati akifungua Mkutano wa 56 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Deus Sangu, amesema mafanikio hayo yametokana na mageuzi ya usimamizi, uwekezaji wenye tija na matumizi ya teknolojia.

Habari Picha 11920

Amesisitiza kuwa Hifadhi Skimu ni nguzo muhimu ya mustakabali wa hifadhi ya jamii nchini, akibainisha kuwa Serikali inalenga kuwafikia Watanzania wengi zaidi, hususan waliojiajiri.

“Upanuzi wa hifadhi skimu ni hatua muhimu ya kuhakikisha hakuna Mtanzania anayebaki nje ya mfumo wa hifadhi ya jamii,” amesema.

Habari Picha 11922

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amesema Mfuko unalenga kufikia thamani ya Sh. Trilioni 24.7 ifikapo Juni 2031 na kuongeza wanachama hadi milioni 6.6, huku ukiimarisha matumizi ya TEHAMA kufikia asilimia 99 ya huduma.

Habari Picha 11923

Ameeleza kuwa mafanikio hayo pia yametokana na utawala bora na uwazi uliowezesha NSSF kupata hati safi ya ukaguzi. Hata hivyo, alibainisha changamoto za baadhi ya waajiri kuchelewesha michango na uelewa mdogo wa hifadhi ya jamii.

Waziri Sangu aliipongeza NSSF kwa uwekezaji katika miradi kama kiwanda cha sukari cha Mkulazi, akisema inachochea ajira na uchumi.

Ameongeza kuwa mipango ya Mfuko inaendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, inayolenga asilimia 70 ya Watanzania kufikiwa na hifadhi ya jamii.

Habari Picha 11924

You Might Also Like

TUCTA Yaitaka Jamii Kuwapa Nafasi Vijana Wenye Changamoto za Kimwili

TUICO Arusha Yapongezwa Na AUWSA

Msigwa Awataka Wakuu Wa Mikoa Kuandaa Maeneo Ya Upandaji Miti

TARURA  Kutoa Fursa Ya Ajira Kwa Vijana

Bunge Marathon kufanyika April 18,yakidhi viwango vya kimataifa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TUCTA: Waajiri Watekeeze Nyongeza Ya Kima cha Mishahara Sekta Binafsi
Next Article Wizara Ya Kilimo Yaomba Bunge Kuidhinisha Trilioni 1.1,Yaweka Mikakati Kuimarisha Sekta Hiyo
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Watendaji Wakuu Waagizwa Kuifanya Dira 2050 Kuwa Mwongozo Wa Maamuzi Yao
Habari July 24, 2026
Nchi za SADC Zahimizwa Kuimarisha Umoja Kukabili Changamoto
Uncategorized July 17, 2026
Wananchi Washauriwa Kutumia  Wataalam Wa Ujenzi Kuepuka Madhara
Habari July 14, 2026
July 14, 2026
Uncategorized July 14, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?