MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TARI Yakutanisha Wadau Afya Ya Udongo
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TARI Yakutanisha Wadau Afya Ya Udongo
Habari

TARI Yakutanisha Wadau Afya Ya Udongo

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: WADAU mbalimbali wa mnyororo wa thamani wa afya ya udongo, wamekutana kubaini changamoto zinazowakabili wakulima ikiwa ni pamoja na kuangalia njia sahihi, endelevu za kutatua.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Dkt.Thomas Bwana akifungua mkutano wa wadau wa kilimo amesema, maabara hai ya afya ya  Udongo inalenga kutatua changamoto mbalimbali za afya ya udongo.
Dkt. Bwana amesema lengo lake  ni kumsaidia mkulima kupata tija bila kuingia gharama zisizo za lazima.
“Tukiwa na uhakika wa afya ya udongo maana yake tunaenda kumsaidia mkulima kutambua namna sahihi ya matumizi ya viuatilifu, mbolea na pembejeo nyingine hata aina ya zao linalofaa eneo husika,” amesema.
Naye Mratibu wa Mradi huo kutoka TARI, Dkt. Atugonza Bilaro amesema wilaya tatu  za Tanzania Bara ikiwemo Kongwa na Babati Mkoa wa Dodoma, Mbozi mkoani Songwe, pamoja na  Zanzibar katika visiwa vya Pemba na Unguja,  ndiko mradi huo utakakofanyika.
Amesema mradi huo  unakuja na njia husishi ya Maabara hai ya afya ya udongo ambayo inajumuisha wataalamu mbalimbali kutoka taasisi tofauti za umma na binafsi wenye lengo moja la kutatua changamoto za afya ya udongo ili kumuongezea mkulima tija.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Norwegian Institute for Bio economy Research (NIBIO), Profesa Udaya Sekhar, amesema suala la  afya ya udongo ni muhimu katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na changamoto mbalimbali zinazosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
Profesa Sekhar amesema kama suala la afya ya udongo halitaangaliwa kwa uzito unaostahili matokeo yake itapunguza tija na
kuhatarisha suala la usalama wa chakula.
TARI imewakutanisha wadau hao ikiwa ni
Hatua ya utekelezaji wa Mradi unaolenga kujenga uwezo wa kitaasisi kwa Watafiti na maofisa ugani, pamoja na mafunzo kwa wakulima juu ya afya endelevu ya udongo katika zama za mabadiliko ya tabianchi.
Mradi huo wa miaka minne kuanzia mwaka 2024 hadi 2027 unatekelezwa na TARI, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar (ZARI,  pamoja na NIBIO kwa ufadhili wa Shirika la maendeleo la Norway (Norad).

You Might Also Like

Majaliwa Aagiza Kuimarishwa kwa Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini

Chalamila: Ujenzi Daraja La Jangwani Waanza

Uongozi OUT Waahidi Kuboresha Mazingira ya Kazi

Tume Ya Kurekebisha Sheria Tanzania Kuipitia Sheria Ya Takwimu

CCM Kuwezesha Wananchi Kufuatilia Mkutano Mkuu Maeneo Ya Wazi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mwanachama Wa TALGWU Akutwa Hana Hatia
Next Article Ridhiwani, Waziri Wa Kazi, Ajira UAE Waweka mkakati
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Tume Ya Ulinzi Wa Taarifa Binafsi Yatoa Siku Saba Kwa Taasisi Kujisajili
Habari June 12, 2026
Teknolojia Ya Juisi YA Ndizi Kali Yafungua Fursa Mpya Za Viwanda, Ajira
Makala Uncategorized June 12, 2026
Serikali Yaingia Makubaliano Ya Ushirikiano Na DIT Kuimarisha Usimamizi Wa Mataifa
Habari June 8, 2026
Wananchi Waelimishwa Masharti ya Kubadilisha Noti Zilizochakaa, Kuungua na Kuchanika
Habari June 7, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?