MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mradi Wa Njia Ya Kusafirisha Umeme Wa Msongo Wa Kilovolti 400 Chalinze -Dodoma Mbioni Kukamilika
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mradi Wa Njia Ya Kusafirisha Umeme Wa Msongo Wa Kilovolti 400 Chalinze -Dodoma Mbioni Kukamilika
Habari

Mradi Wa Njia Ya Kusafirisha Umeme Wa Msongo Wa Kilovolti 400 Chalinze -Dodoma Mbioni Kukamilika

Author
By Author
Share
4 Min Read
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA  la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme ya Msongo wa Kilovolti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma uko kwenye hatua za mwisho za utekelezaji wake, huku ujenzi ukiwa umekamilika kwa asilimia 94 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Agosti 21, 2026.
Akizungumza na waandishi wa habari , Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO,  Irene Gowelle, amesema ili kuwezesha ukamilishaji wa kazi za mradi huo kutakuwepo na katizo la muda la umeme katika baadhi ya maeneo nchini kwa ratiba maalumu kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itakua Julai 30 hadi Agosti 4 na ya pili itaanza Agosti 11 hadi 17, 2026.
Habari Picha 12925
Gowelle amesema hatua hiyo ni sehemu ya maandalizi ya ombi la Mkandarasi anayetekeleza mradi huo kampuni ya TBEA ambayo inalenga kuhakikisha kazi zinafanyika kwa hali ya usalama .
“Mradi huu umefikia hatua muhimu sana ya utekelezaji ambapo kipindi hiki, baadhi ya njia za kusafirisha umeme za kilovolti 220 na 132 zitalazimika kuzimwa kwa muda ili kuruhusu kazi za kuvuta na kuunganisha nyaya mpya kufanyika kwa usalama. Hii ni hatua ya kawaida katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya miundombinu ya kusafirisha umeme na inalenga kukamilisha mradi huu wenye manufaa makubwa kwa Taifa,” amesema  Gowelle.
Habari Picha 12927
Amefafanua kuwa baadhi ya maeneo katika mikoa iliyoko Kanda ya Kati, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Magharibi na Kanda ya Kusini Magharibi inaweza kuathiriwa kwa nyakati tofauti kulingana na ratiba za utekelezaji wa kazi hizo.
 Gowelle amesema TANESCO itaendelea kutoa taarifa kwa wananchi kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na majukwaa mbalimbali ya mawasiliano ili kuwawezesha wateja kupanga matumizi yao ya umeme kwa kuzingatia ratiba zitakazotolewa.
Aidha, amesisitiza kuwa Tanzania ina umeme wa kutosha na kwamba katizo hilo ni la muda, likiwa ni sehemu ya kukamilisha mradi huo wa kimkakati unaolenga kuimarisha uwezo wa usafirishaji wa umeme nchini. Ameongeza kuwa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara haitahusika katika ratiba hiyo ya katizo.
Kwa upande wake, Meneja wa Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme ya Kilovolti 400 Chalinze–Dodoma, Mhandisi Newton Mwakifwamba, amesema mradi huo wenye urefu wa kilomita 345 na thamani ya takribani shilingi bilioni 514 umefadhiliwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema mradi unahusisha ujenzi wa njia mpya ya kusafirisha umeme pamoja na upanuzi wa vituo vya kupokea na kusambaza umeme vya Chalinze na Dodoma.
“Katika hatua hizi za mwisho, tutafanya kazi za kuvusha na kuunganisha njia mpya ya umeme katika maeneo ya Mkambarani, Kikombo na Mkonze. Hatua hizi ni muhimu ili kuhakikisha mradi unaanza kufanya kazi kwa ufanisi na usalama,” amesema Mhandisi Mwakifwamba.
Habari Picha 12928
Ameongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaimarisha uwezo wa mfumo wa taifa wa usafirishaji umeme na kuwezesha usafirishaji wa umeme unaozalishwa katika Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere kwenda maeneo mbalimbali ya nchi, hatua itakayoimarisha uhakika wa upatikanaji wa umeme na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

You Might Also Like

Wahifadhi Saohill Wapongezwa

Mbunge wa Monduli Aahidi Kusimamia Changamoto za Jimbo Lake

Watafiti Mataifa 10 Kujadili ElimuMsingi Nchini

Wadau wa uchukuzi zingatieni maslahi ya wafanyakazi

Katibu Mkuu Uchukuzi Aipongeza TASAC,  Kuelimisha Wananchi 

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kutoka Wazo Rahisi Hadi Mapinduzi ya Kilimo: Safari ya Rafiki Planter Inayosimulia Miaka 40 ya COSTECH
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Kutoka Wazo Rahisi Hadi Mapinduzi ya Kilimo: Safari ya Rafiki Planter Inayosimulia Miaka 40 ya COSTECH
Makala July 28, 2026
Ndejembi Ashuhudia Utiaji Saini Wa Mkataba Wa Sh Bilioni 204.7 Wa Mradi Wa Umeme Wa Jua Wa Megawati 100 Kishapu
Habari July 27, 2026
Watendaji Wakuu Waagizwa Kuifanya Dira 2050 Kuwa Mwongozo Wa Maamuzi Yao
Habari July 24, 2026
Nchi za SADC Zahimizwa Kuimarisha Umoja Kukabili Changamoto
Uncategorized July 17, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?