Na Lucy Lyatuu,Dodoma
WAZIRI wa Kilimo, Daniel Chongolo amewataka wadau wa kilimo nchini kubadilika kwa kuiondoa nchi katika uchuuzi na kuwa ya uzalishaji haswa wa mafuta ya kula na kuondokana na kuagiza kutoka nje ya nchi.
Amesema nchi zinazozalisha mafuta hayo hakuna ilichokizidi Tanzania na kwamba kinachotakiwa ni kuwa na utashi wa kutosha kufikia malengo.
Chongolo amesema hayo katika Jukwaa la Uwekezaji la tasnia ya mafuta ya kula lililoandaliwa kwa pamoja na Mamlaka Ya Udhibiti Wa Nafaka Na Mazao Mchanganyiko (Copra), Benki ya Maendeleo Ya Kilimo Tanzania (TADB) na Benki ya Dunia(WB) lililofanyika jijini Dodoma.

Amesema msimamo wa serikali ndani ya miaka miwili au mwaka mmoja na nusu kuanzia sasa ili uweze kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi lazima kuonesha ulipolima mazao ya alzeti na chikichi ambayo yanazalisha mafuta ya kula.
“Wanaofikiri kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi ndio biashara sasa waanze kuwekeza nchini,” alisema Chongolo na kuongeza kuwa katika miaka miwili ijayo uagizaji wa mafuta ya kula nje ya nchinutakwenda kwa yule aliyewekeza kwenye kilimo kwanza.
Amesema serikali inatoa fedha nyingi kila mwaka kwa ajili ya kuagiza mafuta hayo kutoka nje ya nchi kwa gharama ya dola 200,000 na kuwataka wadau hao kuweka mfumo mkubwa wa kuzalisha mafuta nchini ili kuiitosheleza na kuondoa uhaba uliopo.

Amesema kwa sasa Tanzanianinanuwezo wa kuzalisha tani 300,000 huku mahitaji yakiwa ni tani 700,000 hivyo kuna nakisinya tani 400,000.
Amezitaka taasisi za fedha,wadau wa maendeleo kushirikiana na serikali kaa kutoa mikopo na kuwa na mashamba makubwa ya kulima alzeti na chikichi,mikopo ya kununua vifaa,kupunguza masharti ya dhamana na mikopo yenye riba nafuu kwa wakulima.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TABD Frank Nyabundege amesisitiza uwekezaji wa kina katika zao la chikichi na alzeti na kwamba imetoa mikopo kwa benki ili wadau waweze kutumia fursa hiyo kuzalisha mazao hayo na kuwezesha nchi kujitosheleza.

“Nchi inaagiza mafuta licha ya kuwa na ardhi kubwa na yenye rutuba…taasisi za fedha zitoe mikopo ya fedha tunazowapa ili kuwe na uzalishaji mkubwa wa mafuta ya kula unaofikia tani milioni 1.3 ifikapo mwaka 2030.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Profesa Peter Msofe akimwakilisha Katibu Mkuu Gerald Mweri amesema Wizara imeandaa mkakati wa kuzalisha mafuta na kwamba ifikapo 2035 nchi ijitosheleza.
Amesema mahitaji ya mafuta Tanzania yanaongezeka na serikali inachukua hatua mbalimbali ikiwemo kuongeza utafiti.

