MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Nyavu za Plastiki Zatishia Afya za Watumiaji wa Samaki Ziwa Victoria
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Nyavu za Plastiki Zatishia Afya za Watumiaji wa Samaki Ziwa Victoria
Habari

Nyavu za Plastiki Zatishia Afya za Watumiaji wa Samaki Ziwa Victoria

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi. Mwanza
OFISA Uhifadhi na Uvuvi kutoka taasisi ya Blue Victoria, Alice William, amesema tafiti zinaonyesha kuwa nyavu nyingi za uvuvi zinazotumika katika Ziwa Victoria hutengenezwa kwa plastiki, na zinapoendelea kukaa ndani ya maji hupasuka na kutoa chembechembe ndogo zinazoliwa na samaki, hali inayoweza kuhatarisha afya za binadamu.
Alice amesema samaki wanapomeza chembechembe hizo za plastiki hubaki kwenye misuli yao, na baadaye mlaji wa mwisho ambaye ni binadamu hupata madhara mbalimbali kiafya.
“Nyavu hizi zinapokaa muda mrefu kwenye maji au kupukutika ndani ya maji, hutoa chembechembe za plastiki ambazo samaki huzila. Mwisho wa siku binadamu ndiye anayebeba athari hizo kupitia ulaji wa samaki,” amesema Alice.
Ameeleza kuwa Blue Victoria ni taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na uhifadhi wa bayonuai zilizopo ndani ya Ziwa Victoria, huku shughuli zake zikifanyika katika maeneo ya bonde la ziwa, ikiwemo Mkoa wa Mwanza.
Mbali na uhifadhi wa mazingira, taasisi hiyo pia imekuwa ikiwawezesha wanawake na vijana kuongeza kipato kupitia shughuli za kuongeza thamani ya zao la dagaa.
Amesema wamefanikiwa kujenga vichanja vya kukaushia dagaa katika Kisiwa cha Lukuba pamoja na eneo la Mwalo wa Mswahili jijini Mwanza.
Aidha, amesema taasisi hiyo imeanzisha matumizi ya teknolojia ya kisasa ya sensa (sensor) kwa ajili ya kukusanya taarifa za mazingira ya maji ili kusaidia kutatua tatizo la “kiferezi”, hali ya asili inayotokea ndani ya ziwa kutokana na kupungua kwa kiwango cha oksijeni kwenye tabaka la chini la maji.
Amesema tatizo hilo husababisha samaki aina ya sangara na sato kufa na kuelea juu ya maji, jambo linaloathiri shughuli za uvuvi na uchumi wa wananchi wanaotegemea ziwa hilo.
“Tunatumia sensa kupima hali ya maji mapema kupitia vipimo vya ubora wa maji (water parameters), ili wafugaji na wavuvi waweze kupata tahadhari kabla madhara hayajatokea,” amesema.
Kwa mujibu wa ripoti ya utekelezaji wa miradi ya mwaka 2025, Blue Victoria imefanikiwa kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya nyavu zilizotupwa au kutelekezwa ndani ya ziwa, maarufu kama “ghost nets”.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa watu wengi wamekuwa wakiondoa taka ngumu kama plastiki na makopo lakini huacha nyavu za uvuvi majini bila kujua madhara yake kwa mazingira na afya ya binadamu.
Alice amesema hakuna kiwango salama cha plastiki kinachotakiwa kuwepo katika mwili wa binadamu, huku akionya kuwa hali hiyo inaweza kuchangia magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani.
Kutokana na hali hiyo, taasisi hiyo imeendesha kampeni maalumu za kuondoa nyavu za uvuvi zilizotelekezwa ndani ya Ziwa Victoria ili kupunguza uchafuzi wa mazingira na kulinda afya za wananchi.

You Might Also Like

Bodi Ya  Bima Ya Amana Yapata Mkurugenzi  Mkuu

Tume  Ya Ulinzi  Wa Taarifa Binafsi Yaongeza Muda Wa Taasisi Kujisajili

Wanafunzi 571 watunukiwa Stashahada Na Astashaha Za Vyuo Vya Polisi

Waratibu Wa Kitaifa Wa Nchi Za Jumuiya Ya Ukanda Wa Maziwa Makuu Wakutana Kinshasa

TASAC yahadharisha wavuvi, wasafirishaji majini kuhusu upepo mkali

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Utunzaji Ziwa Victoria Wasisitizwa kwa Mustakabali wa Uchumi, Mazingira
Next Article Ndoinyo Aishauri Serikali Kurejesha Utalii Vijijini
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Uwekezaji wa Vijana Watajwa Chachu ya Ukuaji wa Uchumi
Habari June 29, 2026
Tanzania Yaendelea Kuimarisha Usalama Na Ulinzi Wa Taarifa Binafsi
Habari June 29, 2026
WCF Yapigia Debe Ushirikiano na Teknolojia Kuimarisha Hifadhi ya Jamii
Habari June 28, 2026
Sabasaba 2026 Kuingiza Teknolojia Mpya na Fursa za Uwekezaji
Habari June 27, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?