Na Lucy Lyatuu, Tanga
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam( UDSM),Shule Kuu Ya Sayansi Akua Na Teknolojia Za Uvuvi (SOAF) kimekuja na ubunifu wa dema la kidigitali lenye milango sita katika wiki ya elimu,ubunifu na ujuzi 2026 lenye kumpa nafasi mvuvi kujua idadi ya samaki walioingia.
Mhadhiri Msaidizi wa SOAF,UDSM, Ndalla Missana amesema hayo katika banda la UDSM lililoko katika wiki ya elimu,ujuzi na ubunifu inayoendelea mkoani Tanga katika viwanja vya Usagara.
Amesema kupitia dema hilo mvuvi ataweza kujua kiwango cha samaki walioingia kwa kuwa litakuwa limefungwa kifaa maalum cha kutoa taarifa kwa mvuvi (sensor) kwenye simu yake ya mkononi mara tuu samaki watakapokuwa wameingia.

Amesema hatua hiyo itamrahisishia mvuvi kupungiza muda wa kwenda na kurudi kuangalia dema na atakuwa amekaa sehemu moja huku akipata taarifa kwenye simu kwamba samaki wangapi wameingia kwenye dema lake kwa wakati huo.
“Hivi manake inampa ahueni mvuvi badala ya kwenda na kurudi atakuwa anakwenda mara moja kulitega na atarudi akifuatilia na baaae ataenda kulitoa akiwa na uhakika kama samaki wameingia kwenye mtego” amesema .
Amesema UDSM imefanya utafiti huo kwa muda usiopungua miaka mitatu kuangalia dema hilo,mwanzo walianza kubuni likiwa na aina mojanya umbonla duara na matokeo yakawa sawa na anayopata mvuvi siku zote ndipo walipojaribu ainannhinginenya umbo la nyota lenye milango sita.
Amesema aina hiyo inampa wigo samaki kuingia sehemu yoyote ilimradi aone chakula na kwenhe dema wataweka chakula ambacho sio halisi (artificial) chenye kumvutia samaki akijua ni chakula anachokula na ataingia kupitia mlango wowote kupitia milango hiyo sita.

Ndalla amesema huo mi ubunifu kwa ajilibya kusaidia wavuvi na kwamba UDSM haitoishia hapo bali wanatamani kifaa cha kutoa taarifa kiwe na uwezo wa kupiga picja na kumpa taarifa mvuvi kujua aina ya samaki walioingia.
Amewataka wavuvinkutumia fursa ya wiki hiyo kufika katika banda la UDSM kujifunza nankuhakikisha wanafkkia malengonya Dira ya Taifa Ya Maendeleo 2050.

