MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: eGA Yatengeneza  Mifumo  Kurahisisha  Kazi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > eGA Yatengeneza  Mifumo  Kurahisisha  Kazi
Habari

eGA Yatengeneza  Mifumo  Kurahisisha  Kazi

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Lyatuu
MAMLAKA  ya Serikali Mtandao (eGA) imesema imetengeneza mifumo mbalimbali ya  Teknolojia Ya Habari Na Mawasiliano (TEHAMA) inayosaidia kurahisisha kazi za kila siku serikalini.
Aidha imewawezesha wananchi kupata huduma kwa njia ya kidigitali na kwa urahisi zaidi
Meneja Mawasiliano wa eGA, Subira Kaswaga, amesema hayo  katika maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere,  Dar es Salaam.
Amesema  mamlaka hiyo imepewa jukumu la kisheria kusimamia matumizi ya TEHAMA ndani ya Serikali ili kurahisisha utendaji kazi pamoja na huduma kwa wananchi.
“eGA meendelea kuonesha namna ambavyo Serikali inavyotekeleza mageuzi ya kidigitali kwa lengo la kuboresha utoaji huduma kwa wananchi kupitia matumizi ya TEHAMA,” amesema
Amesema miongoni mwa mifumo hiyo ni mfumo wa e-Mrejesho, ambao ni jukwaa la kidigitali linalowawezesha wananchi kuwasiliana moja kwa moja na Serikali kwa njia ya kupeleka maoni, pongezi au malalamiko, huku Serikali nayo ikijibu na kutoa mrejesho wa hatua zilizochukuliwa.
Amesema mfumo huo unapatikana kwa njia tatu, ikiwemo kupitia simu ya mkononi, na unampa uhuru mwananchi kuficha taarifa zake za msingi iwapo hataki kujulikana, huku pia akipatiwa namba ya ufuatiliaji wa taarifa aliyoitoa.
“Kwa mfumo huu, taasisi za umma zinaweza kuona ni malalamiko ya aina gani zinayapokea mara kwa mara, hivyo kumsaidia kiongozi wa taasisi kutambua idara au kitengo kinachosababisha changamoto kwa wananchi, na kuchukua hatua stahiki,” amesema.
Mbali na hilo, mfumo huu pia unasaidia kupima uwajibikaji wa watendaji wa umma kwa kuruhusu ufuatiliaji wa hatua zinazochukuliwa baada ya malalamiko kuwasilishwa. Viongozi wakuu wa Serikali kama Katibu Mkuu Utumishi na Katibu Mkuu Kiongozi wanaweza kuona kwa uwazi taarifa za malalamiko katika taasisi zote za umma.
Kutokana na mafanikio hayo, Subira amesema kuwa mfumo wa e-Mrejesho umeendelea kuipa sifa Tanzania kimataifa, ambapo Julai 7, 2025, eGA ilishinda tuzo ya kimataifa iliyotolewa na Shirika la ITU katika kipengele cha Serikali Mtandao.
“Ni fahari kubwa kwamba mfumo huu umetengenezwa na Watanzania, na leo unatutambulisha kimataifa. Tunawahamasisha wananchi wauitumie mfumo huu ili Serikali iwafikie kwa urahisi na kwa ufanisi,” amesema.
Amesisitiza kuwa ni wajibu wa watumishi wa umma kuhakikisha kuwa maoni na malalamiko yanayowasilishwa kupitia mfumo huo yanashughulikiwa ipasavyo ili kukuza uwajibikaji na kuongeza imani ya wananchi kwa Serikali.

You Might Also Like

Umeme Jua Kuchoche Uchumi Maeneo Ya Vijijini

VETA Yawasilisha Teknolojia ya Hybrid Katika Maadhimisho ya Wiki ya Vijana

NCCR-MAGEUZI Kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 

Waendelezaji Majengo 103 Kesi Ziko Mahakamani, -AQRB

Wizara Ya Kilimo Yajipanga Vema Maonesho ya Kimataifa Ya Biashara

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article
Next Article TSB Yasisitiza Umuhimu Kuwekeza Kwenye Uchakataji Wa Mkonge
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Kisasa Design: Kampuni ya Kitanzania Inayobadilisha Sekta ya Interior Design na Utengenezaji wa Samani
Habari June 6, 2026
Vidukari Hatari Vyafuatiliwa Mikoa 17 Kulinda Zao la Mpunga
Makala June 5, 2026
KARIBU ESCAPE LODGE SERENGETI – NYUMBA YAKO YA KIFAHARI KATIKATI YA UFALME WA WANYAMAPORI
Habari June 5, 2026
Sheria Ya  Kuzuia Shisha Kutungwa, Yabainika Kuwekwa Dawa Za Kulevya
Habari May 29, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?