Na Lucy Lyatuu,Tanga
MAMLAKA Ya Elimu Na Mafunzo Ya Ufundi Stad (VETA) Pwani imetengeneza simu ya mkononi ambayo kwa sasa ina uwezo wa awali wa kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maandishi.
Mkufunzi wa VETA Kibaha Pwani Hamis Salum amesema hayo katika banda la VETA lililoko katika wiki ya elimu ,ujuzi na ubunifu inayofanyika Tanga katika viwanja vya Usagara.
Amesema simu hiyo imetengenezwa kwa kuanzia kwenye hatua ya moduli kama simu zinavyoundwa na wao wameunda kwa kuunganisha simu mbalimbali.
“Utafiti unatarajia huko mbeleni kutengeneza simu ambayo kama kampuni kubwa za nje zinavyofanya,utafiti huu ulianza mwaka jana”,amesema na kuongeza kuwa kilichomsukuma ni kuona watanzania wanaagiza vitu kutoka nje kukiwa hakuna teknolojia zao wenyewe.

Amesema utengenezaji huo wa simu umeanzia ngazi ya chini ambapo mfumo wa uendeshaji uliopo ndani wametengeneza wenyewe licha ya kwamba wanaingiza baadhi ya vifaa lakini teknolojia nzima inamilikiwa na VETA sio ya nje.
Amesema malenho ni kutengeneza simu kama za kampuni nhingine lakini zimilikiwr na watanzania na kushauri serikali kuendelea kuwekeza kwao na watanzania kwa ujumla walio na bunifu mbalimbali ili kuwe na teknolojia nyingi na kubwa.

