MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: MnyamaTech: Ubunifu Wamtoa Mfugaji Gizani hadi Kidijitali
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Makala > MnyamaTech: Ubunifu Wamtoa Mfugaji Gizani hadi Kidijitali
Makala

MnyamaTech: Ubunifu Wamtoa Mfugaji Gizani hadi Kidijitali

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
10 Min Read
Na Lucy Ngowi
MFUGAJI anaweza sasa kufuatilia afya ya mnyama, kumbukumbu za chanjo na dawa, muda wa uzazi na hata kupata huduma ya daktari wa mifugo kwa kutumia teknolojia ya kidijitali.
Ni suluhisho linalotolewa na MnyamaTech, mfumo uliobuniwa na Kampuni ya Afya ya Mnyama Digital kwa lengo la kutumia teknolojia kuboresha ufugaji na kuongeza thamani ya mifugo katika soko.
Nyuma ya ubunifu huo kuna safari ya mbunifu Maganga Mabula, Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Afya ya Mnyama Digital, ambaye anasema ushirikiano na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) umechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza uwezo wa timu yake na kuimarisha uaminifu wa soko.
Mabula anasema kampuni hiyo ilipofikia hatua ya kuendeleza wazo lake, ilihitaji zaidi ya kuwa na teknolojia, ilihitaji maarifa, mwongozo na mazingira ambayo yangewezesha ubunifu huo kuaminika na kutumika.
“Costech imetusaidia kwanza kabisa kuaminika na taasisi mbalimbali. Kushirikiana nao katika kutuongoza kwenye utengenezaji wa mfumo vizuri, ukusanyaji wa data na kadhalika, kumetuongezea sisi binafsi ujuzi,” anasema.
Kwa mujibu wa Mabula, changamoto kubwa ilikuwa pia kujenga imani ya wateja, hususan mashamba makubwa ambayo yalikuwa bado hayajaamini uwezo wa kampuni hiyo.
Habari Picha 13294
“Baadhi ya mashamba makubwa yalikuwa yanatutia shaka, lakini kupitia kushirikiana na Costech na kuwa chini ya programu yao ya mafunzo, imeanza kutuongezea ‘confidence’ na ‘trust’ kwa upande wa wateja wetu,” anasema.
MnyamaTech imejengwa kwa kuunganisha vifaa vya kidijitali na mfumo unaomwezesha mfugaji kupata taarifa muhimu kuhusu mifugo yake.
Mabula anasema vifaa hivyo vinaweza kufungwa kwa mnyama na kuunganishwa na mfumo ili kusaidia kufuatilia mabadiliko ya hali yake.
Mfumo huo unaweza kumsaidia mfugaji kupata taarifa kuhusu mabadiliko muhimu ya kiafya, ikiwamo dalili za changamoto kabla hazijaonekana kwa nje, pamoja na taarifa kuhusu mnyama anapoingia kwenye joto.
Kwa kufanya hivyo, anasema teknolojia inalenga kumwezesha mfugaji kufanya maamuzi kwa kutegemea taarifa badala ya kusubiri tatizo lijitokeze ndipo aanze kuchukua hatua.
“Mfugaji anaweza kuweka nafasi ya miadi
Kwa daktari au mtoa huduma za wanyama ambaye yuko karibu naye kwa urahisi zaidi,” anasema Mabula.
Na kwa baadhi ya wafugaji, teknolojia hiyo tayari imeanza kubadilisha namna wanavyoshughulikia changamoto za mifugo yao.
Mfugaji kutoka Mkoa wa Pwani, Saraphia Kamwela, anasema MnyamaTech imemsaidia kubaini changamoto za afya ya mifugo na kupata ushauri wa daktari wa wanyama kwa wakati, hasa anapokabiliwa na changamoto ambazo hawezi kuzitatua mwenyewe.
Anasema alianza kutumia mfumo huo Machi mwaka jana 2025,  na tangu wakati huo hajakumbana na changamoto yoyote katika matumizi yake.
“Kwa kweli matumizi yake ni mazuri sana, hasa kwenye upande wa kujua kwamba mnyama anaumwa. Wakati mwingine tunakosa daktari wa wanyama, lakini kupitia mfumo huu ninapopata changamoto, napata daktari wa wanyama kwa urahisi,” anasema.
Kwa Kamwela, matumizi ya teknolojia hiyo yanaonyesha namna teknolojia inaweza kuleta mabadiliko katika ufugaji, hasa kwa wafugaji wanaokabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa wataalamu wa mifugo kwa wakati.
Anawashauri wafugaji wengine kutumia teknolojia hiyo, akisema teknolojia inaendelea kwa kasi na inaweza kusaidia kuboresha ufugaji.
“Badala ya kufuga kienyeji, ni vizuri kutumia teknolojia kwa sababu inasaidia mambo mengi katika ufugaji,” anasema.
Ushuhuda huo unaonyesha namna ubunifu unaotengenezwa na Mtanzania unavyoweza kutoka katika hatua ya wazo na kuanza kutumika kutatua changamoto halisi zinazowakabili wananchi.
Mbali na ufuatiliaji wa afya, mfumo huo unamwezesha mfugaji kuhifadhi kumbukumbu za mifugo yake, zikiwamo taarifa za chanjo, dawa za minyoo na huduma nyingine zilizotolewa.
Mfumo unaweza pia kumkumbusha mfugaji muda wa kurudia chanjo au kutoa huduma nyingine muhimu.
Katika uzazi, teknolojia hiyo inaweza kusaidia kufuatilia muda unaotarajiwa wa mnyama kuzaa na kutoa ukumbusho kabla ya wakati huo.
Kwa mtazamo wa Mabula, taarifa hizo si muhimu kwa afya pekee, bali pia zinaweza kuwa sehemu ya kuongeza thamani ya mnyama katika soko.
MnyamaTech inalenga kuifanya taarifa ya mnyama kuwa sehemu ya biashara yake.
Kupitia taarifa zinazokusanywa, mfugaji anaweza kuwa na kumbukumbu zinazohusu historia ya mnyama, alikofugwa na huduma alizowahi kupata.
Taarifa hizo zinaweza kumsaidia mnunuzi kufanya uamuzi akiwa na uelewa mpana zaidi kuhusu mnyama anayenunua.
Hatua hiyo inalenga kuongeza uwazi na uaminifu katika biashara ya mifugo, huku teknolojia ikitoa nafasi ya kubadilisha taarifa za afya na historia ya mnyama kuwa sehemu ya thamani yake sokoni.
Habari Picha 13294
Mfumo huo pia unalenga kuwahudumia madaktari wa mifugo, watoa huduma na wafanyabiashara wa dawa za mifugo.
Mtoa huduma za mifugo anapojisajili, anatakiwa kuwasilisha uthibitisho unaohitajika kutoka mamlaka husika, huku wafanyabiashara wa maduka ya dawa za mifugo wakiwasilisha nyaraka zinazothibitisha biashara zao.
Kwa upande wa wafanyabiashara hao, mfumo unaweza kusaidia kutunza kumbukumbu za duka, bidhaa zilizopo, matumizi na taarifa nyingine za biashara.
Kampuni inapatikana kupitia majukwaa ya kidijitali na tovuti yake, huku ikishirikiana na wataalamu wa mifugo kuwasaidia watumiaji kuelewa namna ya kutumia mfumo.
Kwa miaka 40, COSTECH imekuwa ikitekeleza jukumu la kuratibu na kuendeleza sayansi, teknolojia na ubunifu nchini.
Meneja wa Ubunifu na Teknolojia wa COSTECH, Gerald Kafuku, anasema jukumu la taasisi hiyo ni kuhakikisha mazingira yanamwezesha mbunifu kutoka katika hatua ya wazo hadi kufikia bidhaa au huduma inayoweza kutumika katika jamii na kuuzwa sokoni.
“Costech ni shirika la Serikali linalofanya kazi ya kuratibu na kuendeleza sayansi na teknolojia nchini. Tunafanya kazi kwa kutoa msaada wa kitaalamu, msaada wa kifedha, pamoja na kuwaunganisha watumiaji wa teknolojia na wazalishaji wa teknolojia,” anasema.
Anasema msaada huo unaelekezwa zaidi kwa wabunifu ambao wamefikia hatua ambayo mawazo yao yanaweza kuendelezwa na kufikia bidhaa au huduma inayoweza kutumika.
“Si wale ambao wana mawazo ambayo bado hayajafika. Hawa hapa wana ubunifu ambao umefikia hatua ambayo tunaweza kutengeneza bidhaa nyingine, tunaweza kuwapatia msaada wa kitaalamu na kifedha ziende kutumika kwenye soko kama bidhaa zinazouzwa,” anasema.
Kwa maelezo hayo, safari ya MnyamaTech inaingia ndani ya dhana pana ya Costech ya kuhakikisha ubunifu hauishii kwenye wazo, bali unafika kwenye matumizi.
Kafuku anasema ubunifu ni mchakato unaoweza kuanzia kwenye wazo jipya au kuboresha wazo lililopo na kulifikisha katika hatua ya bidhaa, huduma, mchakato au njia mpya ya kufanya kazi.
“Ubunifu ni hatua ya kutoa wazo ambalo linafikia kwenye bidhaa ambayo inaweza kuwa bidhaa, inaweza kuwa mchakato au mchakato, inaweza kuwa mbinu au njia za kufanya kazi. Inaweza kuwa wazo jipya kabisa au wazo ambalo lipo, lakini mtu ameliboresha na kulipatia hatua,” anasema.
Kwa msingi huo, Costech imeendelea kutoa msaada wa kitaalamu na kifedha kupitia programu zake, huku wabunifu wakiomba na kuchaguliwa baada ya kufanyiwa mchakato wa uchambuzi kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa.
Costech pia hushirikiana na taasisi nyingine za utafiti na vituo vya ubunifu, pamoja na wadau wa maendeleo wanaosaidia kupanua fursa kwa wabunifu.
Kafuku anataja taasisi za kimataifa ikiwamo Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kuwa miongoni mwa wadau wanaoshiriki katika programu mbalimbali za kuendeleza ubunifu.
Kafuku anasema vijana ni miongoni mwa kundi linalotumia kwa kasi maarifa na taarifa za teknolojia kutoka sehemu mbalimbali duniani na kuzibadilisha ili kukidhi mahitaji ya mazingira ya Tanzania.
“Vijana wanachukua hizo taarifa za kibunifu, wanazifanya katika mazingira ya Tanzania,” anasema.
Hali hiyo inaonyesha nafasi ya teknolojia katika kuwawezesha Watanzania kutengeneza majibu ya changamoto zao wenyewe kwa kutumia maarifa yaliyopo duniani na kuyabadilisha kulingana na mazingira ya ndani.
MnyamaTech ni sehemu ya simulizi hiyo, wazo lililojengwa kutoka kwenye changamoto za ufugaji na kugeuzwa kuwa mfumo unaolenga kuleta taarifa, huduma na ufanisi zaidi katika sekta ya mifugo.
Kwa Costech, maadhimisho ya miaka 40 si kumbukumbu ya taasisi pekee, bali ni nafasi ya kuangalia namna sayansi, teknolojia na ubunifu ulivyoweza kuingia katika maisha ya wananchi.
Kwa upande wa Afya ya Mnyama Digital, ushirikiano huo umeonyesha kwamba kwa mbunifu, msaada hauishii kwenye fedha.
Unahusisha pia maarifa, mwongozo wa kitaalamu, kujenga uwezo, kuaminika na kupata mazingira ya kuunganisha teknolojia na mahitaji ya soko.
Hapo ndipo safari ya MnyamaTech inakuwa zaidi ya hadithi ya mfumo wa kidijitali wa mifugo; inakuwa mfano wa namna wazo la Mtanzania linavyoweza kupewa nafasi ya kukua na kutafuta suluhisho la changamoto inayogusa maisha ya wananchi.
Kwa Mabula, lengo ni kuona teknolojia ikiingia zaidi katika ufugaji, mfugaji akiwa na taarifa sahihi kuhusu mnyama wake na biashara ya mifugo ikijengwa juu ya uwazi na uaminifu zaidi.
“Karibuni tufuge kidijitali,” anasema Mabula.

You Might Also Like

MATUKIO YALIYOJIRI KUANZIA JANUARI 2024, HADI SASA DISEMBA 2024:

Mwelekeo Mpya wa Viwanda: Safari ya Siku 100 za Mageuzi ya Kiuchumi

Tujenge Jumuiya Yenye Mustakabali wa Pamoja kati ya China na Afrika – Wang Yi

Rais CWT Ni Kiongozi Aliyekuza Taaluma Kwa Moyo, Sio Cheo

Shilingi Milioni 28 Zilivyogeuza Wazo Kuwa Mashine Ya Shambani

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Waziri Mkenda Kuzindua Wiki Ya Elimu,Ujuzi Na Ubunifu,Washiriki Takriban 300 Waonesha Bunifu Mbalimbali
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Waziri Mkenda Kuzindua Wiki Ya Elimu,Ujuzi Na Ubunifu,Washiriki Takriban 300 Waonesha Bunifu Mbalimbali
Habari August 17, 2026
VETA Kibaha Yatengeneza Simu Ya Mkononi Yenye Uwezo Wa Kupiga Na Kutuma Sms
Habari August 17, 2026
Wiki Ya Elimu, Ujuzi Na Ubunifu,UDSM Yabuni Dema La Kidigitali La Milango Sita Kusaidia Wavuvi
Habari August 17, 2026
TTCL  Yatumia Tamasha La Kizimkazi Kueleza  Wananchi Fursa Wanazotoa
Makala August 15, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?