MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TARURA  Kutoa Fursa Ya Ajira Kwa Vijana
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TARURA  Kutoa Fursa Ya Ajira Kwa Vijana
Habari

TARURA  Kutoa Fursa Ya Ajira Kwa Vijana

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Lucy Lyatuu, Dodoma

WAKALA wa Barabara Vijijini  Na Mijini (TARURA) umesema  kuelekea utekelezaji wa  dira 2050 inawapatia ajira vikundi vya vijana, wanawake na walemavu ambapo inatoa elimu kwa wananchi waweze  kufanya kazi za barabara .
Mkuu wa Kitengo  cha Uhusiano Na Mawasiliano TARURA, Catherine Sungura amesema hayo wakati akizungumza katika banda la Wakala huo, lililopo katika  wiki ya utumishi wa umma  yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park mkoani Dodoma.
Amesema programu hiyo ni ya nchi nzima  kasoro mkoa wa Dar es Salaam na imeanza katika miaka miwili iliyopita ambapo kupitia elimu wamewafikiwa vikundi vya vijana,wanawake na walemavu.
Amesema kupitia vikundi hivyo, husajiliwa  kwenye mfumo wa NeST na iwapo ikitokea zabuni ya ujenzi wa barabara au madaraja hupewa  kazi za matengenezo madogomadogo  kwa mwaka mara moja.
Habari Picha 12495
“Kama wamepewa barabara fulani huifanyia matengenezo  madogomadogo,hata kama kuna mfereji wenye mchanga hupewa zabuni waifanye kwa mwaka mzima,” amesema Catherine  huku akitolea mfano kikundi  cha waendesha bodaboda kilichoko Ifakara kuwa kimeweza kujinufaisha kwa program hiyo.
Amesema kikundi hicho kimepata takriban sh milioni 13 kwa kusafisha barabara  ambayo ni fursa ya ajira kwa vijana, hivyo anatoa wito kwa wananchi kujiunga na kuchangamkia fursa hiyo
Catherine amesema mfano mwingine ni kikundi kilichopo Ludewa ambapo kilianza siku nyingi kwa kujenga barabara wameweza kununua pikipiki, kuweka mizinga ya asali ambapo hukopeshana na kuongeza mitaji.
Kwa upande wake Ofisa Utumishi Mkuu wa TARURA,  Speransia Mhapa amesema wakala huo umefanikiwa kufungua nchi katika maeneo mbalimbali kwa ujenzi wa barabra na kutoa huduma.
Amewakaribisha wananchi katika banda hilo waulize na kutoa mirejesho ya kazi za wakala huo na kuiwezesha Tarura kujifanyia tathmini kuhusu huduma watoazo.

You Might Also Like

Mbunge Ngorongoro Aiomba Serikali Kufungua Uchumi Loliondo

Mwanachama Wa TALGWU Akutwa Hana Hatia

Ulega Ataka Ushirikiano Miradi Ya Kimkakati Ikamilike Kwa Wakati

Washauri Serikali Kutumia Fedha Za Miradi

Tanzania Kuwa Mwenyeji Wa Mkutano Wa Petroli Afrika

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article DCF Atembelea Banda Wizara Mambo YA Nje, Atoa Pongezi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

DCF Atembelea Banda Wizara Mambo YA Nje, Atoa Pongezi
Habari June 20, 2026
June 20, 2026
Uncategorized June 20, 2026
PSSSF Yafanya Maisha Kuwa Rahisi Kwa Wanachama
Habari June 20, 2026
Serikali Yaitaka TBS Kuongeza Ubunifu, Usasa
Habari June 20, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?