MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wizara Ya Kilimo Yaomba Bunge Kuidhinisha Trilioni 1.1,Yaweka Mikakati Kuimarisha Sekta Hiyo
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wizara Ya Kilimo Yaomba Bunge Kuidhinisha Trilioni 1.1,Yaweka Mikakati Kuimarisha Sekta Hiyo
Habari

Wizara Ya Kilimo Yaomba Bunge Kuidhinisha Trilioni 1.1,Yaweka Mikakati Kuimarisha Sekta Hiyo

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Lucy Lyatuu

KATIKA mwaka wa fedha 2026/27, Serikali  imeweka mikakati 30 ya kimkakati inayolenga kuimarisha sekta ya kilimo nchini  huku ikidhamiria kuongeza uzalishaji wa zao la miwa kutoka Tano 4351673.1 hadi tani 5500,000.

Aidha Wizara hiyo imeomba kuidhinishiwa trilioni 1,105,950,115  jambo litakalowezesha  kuongeza tija na uzalishaji, kuchochea ajira kwa vijana na wanawake, pamoja na kuimarisha usalama wa chakula na lishe kwa wananchi.

Waziri wa Kilimo,Daniel Chongolo amesema hayo  bungeni Dodoma na Waziri wa Kilimo, wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Kuhusu mikakati hiyo, Chongolo  amesema Wizara  imejipanga kutekeleza mikakati hiyo katika maeneo manne makuu yanayolenga kubadili taswira ya sekta ya kilimo nchini.

Kuhusu  zao la miwa na uzalishaji wa sukari amesema tani 4351673.1 zilizozalisha sukari tani 410979…04 mwaka 2025/26 hadi tani 5500,000 za miwa zitakazozalisha sukari tani 550,000.

Amesema vile vile Wizara kupitia TARI itaanzisha shamba la kuzalisha mbegu za miwa Lenye ukubwa wa ekari 10  katika Halmashauri ya Kilosa ambalo litakuwa na uwezo wa kuzalisha jumla ya tani 400 za mbegu za miwa.

Kuhusu kuongeza tija na uzalishaji, Serikali imeelekeza nguvu katika utafiti wa kilimo, uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora na miche, pamoja na utoaji wa ruzuku ya mbolea, mbegu na viuatilifu kwa wakulima. 

“Mikakati mingine ni pamoja na usajili wa wakulima, kuimarisha huduma za ugani, kuanzisha mashamba makubwa ya pamoja na kupima afya ya udongo, pamoja na kuendeleza kilimo cha umwagiliaji na vituo vya huduma za zana za kilimo,”amesema.

Kuhusu  kuhakikisha usalama wa chakula na lishe nchini, Serikali imepanga kuwekeza katika miundombinu ya uhifadhi wa chakula ili kufikia uwezo wa kuhifadhi tani milioni 3 ifikapo mwaka 2030. Aidha, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) utaongezewa uwezo wa kununua mazao ya wakulima kwa wingi zaidi.

Kuhusu Kuwezesha Upatikanaji wa Mikopo kwa Vijana na Wanawake (BBT Mitaji)  amesema Wizara kupitia Mfuko wa Dhamana wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) itawezesha upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu ya Sh Bilioni tano kwa vijana na wanawake. 

Vilevile,amesema Wizara itaweka kiasi cha Dola za Marekani Milioni 35 kwenye Benki za biashara kwa ajili ya guarantee scheme zitakazowezesha vijana na wanawake kupata 186 mikopo yenye riba nafuu mara mbili au zaidi ya fedha hizo. 5.2.4 

Aidha Kuhusu Kuwezesha Vijana na Wanawake Kuongeza Thamani ya Mazao amesema Wizara kupitia Bodi ya Mkonge itaendelea kutoa mafunzo ya kuongeza thamani ya zao la mkonge kwa vijana na wanawake 200 ili waweze kuzalisha bidhaa zitokanazo na zao hilo.

; 

You Might Also Like

TRC, Wananchi Burundi Wakutana Utekelezaji Mradi wa SGR

VETA Yatahadharisha Changamoto ya Kuzidisha Uchanganyaji wa Chakula Cha Mifugo

Wananchi wa Kasulu Vijijini Wananufaika na Uwekezaji Makere Forest Reserve

Tanzania, UAE Kuimarisha Ushirikiano Wa Kibunge

DIB: Wenye Amana Benki Zilizofungwa Kulipwa Ndani ya Mwezi Mmoja

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article NSSF Yafikia Trilioni 11.2, Hifadhi Skimu Yatajwa Kubadili Maisha ya Watanzania
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yafikia Trilioni 11.2, Hifadhi Skimu Yatajwa Kubadili Maisha ya Watanzania
Habari April 27, 2026
TUCTA: Waajiri Watekeeze Nyongeza Ya Kima cha Mishahara Sekta Binafsi
Habari April 27, 2026
Serikali Yaweka Mkazo Kufufua Viwanda Musoma Ili Kuongeza Ajira
Habari April 24, 2026
Program Ya Mama Samia Ya Kurasimisha Ujuzi Yazinduliwa
Habari April 23, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?