MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: NeST Yaongeza Uwazi Na Ufanisi Katika Ununuzi Wa Umma
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > NeST Yaongeza Uwazi Na Ufanisi Katika Ununuzi Wa Umma
Habari

NeST Yaongeza Uwazi Na Ufanisi Katika Ununuzi Wa Umma

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dennis  Simba, amesema matumizi ya Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa Njia ya Kielektroniki (NeST) yameleta mageuzi makubwa katika sekta ya ununuzi wa umma nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari  Dodoma, Simba amesema mfumo huo umewezesha Serikali kuongeza ufanisi katika michakato ya ununuzi, kupunguza muda wa kushughulikia zabuni pamoja na kuongeza uwazi na usawa kwa wazabuni.
Amesema takribani asilimia 70 ya bajeti yote ya Serikali hutumika kupitia ununuzi wa umma, hivyo mfumo huo unatoa fursa kwa wananchi, wajasiriamali na wazabuni kushiriki katika shughuli za Serikali kwa njia iliyo wazi na yenye ushindani.
“Mfumo wa NeST umekuja na mabadiliko makubwa katika sekta ya ununuzi wa umma, kwa kuongeza uwazi, ufanisi na kupunguza gharama za michakato ya ununuzi,” amesema Simba.
Ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ilitoa msukumo wa matumizi ya teknolojia katika kuboresha usimamizi wa sekta ya ununuzi wa umma, hatua iliyowezesha NeST kuanza kutumika rasmi mwaka 2023.
Kwa mujibu wa Simba, kwa sasa mfumo huo una moduli sita ambazo ni usajili wa watumiaji (e-Registration), uendeshaji wa zabuni (e-Tendering), usimamizi wa mikataba (e-Contract Management), malipo (e-Payment), katalogia (e-Catalogue) pamoja na minada ya kielektroniki (e-Auction).
Amesema kupitia NeST, shughuli za ununuzi wa umma zinafanyika kwa njia ya kidijitali, jambo linalopunguza matumizi ya karatasi, gharama za usafiri na muda unaotumika katika michakato ya zabuni, huku pia likiongeza ufuatiliaji na uwajibikaji.
“Hatua hii imewezesha kuondoa kabisa uhusiano wa kuwa na nyaraka za kughushi kwenye mfumo, lakini pia kurahisisha mchakato wa kuwasilisha nyaraka husika wakati wa michakato ya zabuni,” amesema Simba.
Aidha, amesema PPRA inaendelea na hatua za kuunganisha NeST na mifumo mingine ya Serikali, ikiwemo mifumo ya malipo na benki, ili kuongeza ufanisi na kuhakikisha michakato ya ununuzi wa umma inakuwa salama, ya haraka na yenye uwazi zaidi.

You Might Also Like

WRRB Kuanza Kuingiza Sekta Ya Mifugo Kwenye Mfumo Wa Stakabadhi Za Ghala

Tanzania, Afrika Kusini Zakubaliana Kuharakisha Makubaliano ya Ushirikiano

TPDC Kufikisha Gesi Nchi Nzima  Ndani Ya Miaka Miwili Na Nusu  Kuanzia Sasa

VETA Yatembelea Kiwanda Cha Kutengeneza Nyumba Bila Kutumia Tofali

Udongo wa kupandia mboga mboga unapatikana VETA

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Miaka 40 ya COSTECH: Teknolojia Yafungua Milango ya Elimu kwa Wasioona
Next Article Tanzania Yanoa Vijana Kuwa Mabingwa Wa Ujuzi Afrika,Duniani Kupitia WorldSkills
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Tanzania Yanoa Vijana Kuwa Mabingwa Wa Ujuzi Afrika,Duniani Kupitia WorldSkills
Habari August 20, 2026
Miaka 40 ya COSTECH: Teknolojia Yafungua Milango ya Elimu kwa Wasioona
Makala August 20, 2026
Mkenda: Bunifu Zigeuke Bidhaa Na Biashara
Habari August 20, 2026
Barabara Zinazopasuka, Suluhisho Linalotoka Maabara za Tanzania
Makala August 19, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?