MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: WRRB Kuanza Kuingiza Sekta Ya Mifugo Kwenye Mfumo Wa Stakabadhi Za Ghala
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > WRRB Kuanza Kuingiza Sekta Ya Mifugo Kwenye Mfumo Wa Stakabadhi Za Ghala
Habari

WRRB Kuanza Kuingiza Sekta Ya Mifugo Kwenye Mfumo Wa Stakabadhi Za Ghala

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Lyatuu,Dodoma
BODI Ya Usimamimazi Wa Stakabadhi Za Ghala (WRRB ) ina mpango wa kuanza kuingiza sekta ya mifugo kwenye Mfumo wa Stakabadhi za Ghala ni hatua mpya ya kihistoria ambayo inalenga kutoa suluhu kwa wafugaji nchini.
Kwa miaka 20 iliyopita mfumo huu umekuwa ukitumika zaidi kwenye mazao ya kilimo kama mahindi, pamba na korosho.
Habari Picha 12948
Kwa sasa WRRB   imeamua kupanua wigo wake ili  wafugaji waweze kunufaika na mikopo nafuu na masoko ya uhakika kupitia dhamana ya bidhaa zao.
 Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB,  Asangye Bangu, amesema hayo wakati akizungumzia  utekelezaji wa miradinya maendeleo  kwa mwaka wa fwdha 2025/26 na mwelekeo wa fedha 2026/27.
Kuhusu mkakati wa Bodi kwa miaka mitano ijayo kuanzia 2027 hadi 2031 inapanua wivo wa mfumo wa bidhaa lakini pia kuanza kuinhiza sekta ya mifugo.
Amesema  uamuzi huu umetokana na mahitaji makubwa kutoka kwa wafugaji katika mikoa ya kanda ya kati, kaskazini na kusini mwa nchi.
Habari Picha 12949
“Wafugaji wengi wamekuwa wakilazimika kuuza mifugo yao kwa bei ndogo wakati wa kiangazi kutokana na ukosefu wa malisho na mtaji. Kwa kuingiza ngozi ghafi, nyama iliyohifadhiwa, maziwa yaliyosindikwa na malisho ya mifugo kwenye mfumo, wafugaji sasa wataweza kuhifadhi bidhaa zao na kupata mkopo wa hadi asilimia 70 ya thamani yake,” amesema.
Amesema  kama sehemu ya kuanzisha mfumo huo, WRRB inashirikiana na wizara ya mifugo na uvuvi pamoja na benki za kibiashara kuweka viwango vya ubora na maghala maalum ya kuhifadhia bidhaa za mifugo.
Maghala hayo yatakuwa na vyumba vya baridi, maeneo ya kukausha ngozi, na hifadhi za malisho. Mfugaji akileta bidhaa zake atapewa stakabadhi ya kielektroniki ambayo anaweza kuitumia kupata mkopo au kuuza katika soko la bidhaa.
  “Faida kubwa ya mpango huu ni kuondoa adha ya wafugaji kuuza kwa hasara. Kwa sasa msimu wa ukame ukifika bei ya ng’ombe na mbuzi hushuka kwa zaidi ya asilimia 50. Lakini kwa mfumo mpya, mfugaji anaweza kusubiri hadi bei ipande sokoni bila kuogopa kuharibika kwa bidhaa yake. Aidha, benki zitapata uhakika zaidi wa kutoa mikopo kwa sababu stakabadhi itakuwa dhamana rasmi iliyosajiliwa na serikali,” amesema.
Amesema kwa ujumla, kuingizwa kwa sekta ya mifugo kwenye Mfumo wa Stakabadhi za Ghala ni mwanzo wa enzi mpya ya mageuzi katika kilimo cha mifugo nchini.
Habari Picha 12950
“Serikali kupitia WRRB inaamini kwamba hatua hii itaongeza mchango wa sekta ya mifugo kwenye Pato la Taifa, kuboresha maisha ya wafugaji, na kuifanya Tanzania kuwa na mfumo imara wa chakula na malighafi kwa viwanda. WRRB sasa inatamka wazi: hakuna tena mfugaji atakayelazimika kuuza kwa bei ya hasara,”amesema.
Kuhusu mikakati mipya ya WRRB kwa mwaka wa fedha 2026/27  amesema inalenga kuimarisha Mfumo wa Stakabadhi za Ghala na kuufanya kuwa mhimili mkuu wa uhakika wa masoko na upatikanaji wa mitaji kwa wakulima wadogo na wakubwa.

You Might Also Like

Miradi Ya Kusambaza Umeme Vitongojini Kukamilika Ifikapo 2030

Miradi Dodoma Yamkuna Rais Samia

Samia Mgeni Rasmi Siku Ya Mashujaa

Waziri Mkuu Mstaafu Pinda Atoa Neno Kwa Vijana, Maadhimisho Miaka 30 VETA

Mbegu Bora za Miwa Zenye Tija ya Tani 200 kwa Hekta Zaendelea Kuwanufaisha Wakulima

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wadau Wa Kilimo Iondoeni Nchi Kwenye Uchuuzi Wa Mafuta Ya Kula-Chongolo
Next Article  Wanasheria Wa TANESCO Watakiwa Kuendelea Kusimamia Maadili Na Taaluma-Twange
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

 Wanasheria Wa TANESCO Watakiwa Kuendelea Kusimamia Maadili Na Taaluma-Twange
Habari July 31, 2026
Wadau Wa Kilimo Iondoeni Nchi Kwenye Uchuuzi Wa Mafuta Ya Kula-Chongolo
Habari July 30, 2026
Wadau Wa Kilimo Iondoeni Nchi Kwenye Uchuuzi Wa Mafuta Ya Kula-Chongolo
Habari July 30, 2026
Mradi Wa Njia Ya Kusafirisha Umeme Wa Msongo Wa Kilovolti 400 Chalinze -Dodoma Mbioni Kukamilika
Habari July 29, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?