MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Tanzania Yanoa Vijana Kuwa Mabingwa Wa Ujuzi Afrika,Duniani Kupitia WorldSkills
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Tanzania Yanoa Vijana Kuwa Mabingwa Wa Ujuzi Afrika,Duniani Kupitia WorldSkills
Habari

Tanzania Yanoa Vijana Kuwa Mabingwa Wa Ujuzi Afrika,Duniani Kupitia WorldSkills

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Lyatuu, Tanga
SERIKALI imesema inaendelea kuwaandaa vijana wa Kitanzania wenye ujuzi na vipaji mbalimbali ili kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya ujuzi ya Afrika na baadaye dunia kupitia mfumo wa WorldSkills.
Imesema hatua hiyo ,  ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha elimu inayozingatia ujuzi na mahitaji ya soko la ajira.
Akizungumza  katika Wiki ya Elimu, Ujuzi Na Ubunifu 2026  Sayansi, inayofanyika jijini Tanga, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profssa Carolyne Nombo, amesema Serikali inatumia mbinu mbalimbali kuwajengea wanafunzi ujuzi wa vitendo.
Amesema mafunzo hayo yanahusiana,  kuwatoa darasani na kuwapeleka katika mazingira halisi ya kazi pamoja na kuwashirikisha katika mashindano ya ujuzi yanayoratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTVET).
Habari Picha 13325
Profesa Nombo amesema Tanzania, baada ya kuwa mwanachama wa mfumo wa WorldSkills, imeanza kuweka mazingira ya kuibua na kukuza vijana wenye vipaji na ujuzi kuanzia mashindano ya ngazi za chini hadi kufikia majukwaa ya kimataifa.
Amesema vijana wanaoshiriki mashindano hayo ni miongoni mwa waliothibitisha uwezo katika fani zao na wanaendelea kutathminiwa ili kubaini watakaoiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Afrika na baadaye dunia.
Amesema maandalizi ya vijana hao yanahitaji ushirikiano wa Serikali, taasisi za elimu, wataalamu na sekta binafsi, kwa kuwa hakuna upande mmoja unaoweza kufanikisha lengo hilo.
 Profesa Nombo amesema wataalamu kutoka taasisi mbalimbali, zikiwamo taasisi za mafunzo ya ufundi na utalii, wamekuwa wakishiriki kuwaandaa vijana kwa kuzingatia viwango vinavyotumika katika mashindano ya kimataifa.
Habari Picha 13326
Kwa mujibu wa Profesa Nombo, wataalamu kutoka Tanzania pia wanapata uzoefu kuhusu namna mashindano ya kimataifa yanavyoendeshwa, mifumo ya tathmini na maandalizi ya washiriki.
“Baadhi ya wataalamu tayari wamepata mafunzo kutoka kwa wadau wa mashindano ya ujuzi ya kimataifa, hivyo mashindano yanayoendelea nchini yanaandaliwa kwa kuzingatia vigezo vya kimataifa,” amesema.
Katika hatua nyingine, Profesa Nombo amesema Serikali inaendelea kusimamia elimu jumuishi kwa kuhakikisha vijana wenye mahitaji maalum wanapata fursa ya kuonyesha vipaji na uwezo wao.
Amesema ushiriki wao katika mashindano hayo unaonyesha kuwa changamoto za ulemavu si kikwazo cha kutumia kipaji na kuchangia maendeleo ya taifa, huku Serikali ikilenga kujenga kundi la vijana wenye ujuzi wa hali ya juu watakaoweza kushindana na wenzao Afrika na duniani.

You Might Also Like

Viongozi Bora Hujenga Mazingira Wezeshi Kwa Wahadhiri – Profesa Nombo

SEforALL Kuimarisha Ushirikiano Upatikanaji Nishati Endelevu

Msigwa Awataka Wakuu Wa Mikoa Kuandaa Maeneo Ya Upandaji Miti

MBUNGE wa Kasulu Mjini Ahoji Serikali Kuhusu Mradi wa Maji Mwanga B

Dar Yaidhinishiwa Bil. 68 Ukarabati, Matengenezo Ya Barabara

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article NeST Yaongeza Uwazi Na Ufanisi Katika Ununuzi Wa Umma
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NeST Yaongeza Uwazi Na Ufanisi Katika Ununuzi Wa Umma
Habari August 20, 2026
Miaka 40 ya COSTECH: Teknolojia Yafungua Milango ya Elimu kwa Wasioona
Makala August 20, 2026
Mkenda: Bunifu Zigeuke Bidhaa Na Biashara
Habari August 20, 2026
Barabara Zinazopasuka, Suluhisho Linalotoka Maabara za Tanzania
Makala August 19, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?