MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Barabara Zinazopasuka, Suluhisho Linalotoka Maabara za Tanzania
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Home » Tovuti » Barabara Zinazopasuka, Suluhisho Linalotoka Maabara za Tanzania
Makala

Barabara Zinazopasuka, Suluhisho Linalotoka Maabara za Tanzania

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
9 Min Read
Na Lucy Ngowi
BARABARA inapopasuka muda mfupi baada ya kujengwa, kinachopasuka si lami pekee.
Pamoja nayo hupasuka fedha za umma zilizotumika kuijenga, muda wa wasafirishaji, biashara za wananchi na matumaini ya jamii iliyotarajia miundombinu hiyo ibaki imara kwa miaka mingi.
Katika Tanzania inayojenga barabara, nyumba, madaraja na miundombinu mingine kwa kasi, swali la muhimu si kujenga pekee, bali ni kujenga kwa teknolojia gani ili miundombinu idumu, gharama zipungue na mazingira yalindwe?
Jibu moja limeanza kutengenezwa ndani ya maabara za Tanzania.
Ni ubunifu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) unaolenga kubadili namna baadhi ya vifaa vya ujenzi vinavyotengenezwa na kutumika, kupitia teknolojia za Duracem, Duracem 1A na Novacem.
Huu si ubunifu unaolenga kubaki kwenye maabara. Ni utafiti unaolenga kuvuka mpaka wa chuo na kuingia kwenye barabara, majengo na shughuli za kila siku za Watanzania.
Kwa mwananchi wa kawaida, barabara si suala la uhandisi pekee.
Habari Picha 13305
Ni njia ya mtoto kwenda shule, mkulima kufikisha mazao sokoni, mfanyabiashara kusafirisha bidhaa na mgonjwa kufika hospitalini kwa wakati.
Barabara inapoharibika, athari zake huenea katika maisha yote hayo.
Ndiyo maana utafiti unaolenga kuongeza uimara wa miundombinu una umuhimu unaozidi maabara na vyuo vikuu.
Akizungumza katika Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, Mkurugenzi wa Idara ya Kemia wa UDSM
Dkt. Makungu Madirisha,  anasema teknolojia hizo zimetokana na tafiti zinazofanywa na watafiti wa chuo hicho kwa lengo la kutafuta suluhisho za changamoto zinazowakabili Watanzania.
Miongoni mwa bidhaa hizo ni Novacem, saruji mbadala inayoweza kutumika katika kutengeneza bidhaa mbalimbali za ujenzi, zikiwemo matofali na paving.
Kisha kuna Duracem, inayolenga matumizi katika tabaka za barabara, pamoja na Duracem 1A, ambayo hutumika kama kionjo katika mchanganyiko wa lami.
“Duracem inatumika sana katika kujenga tabaka la juu na tabaka la chini la barabara. Duracem 1A ni kionjo kinachochanganywa na lami mbalimbali,” anasema.
Kwa mujibu wa UDSM, Duracem na Duracem 1A zilitengenezwa kama teknolojia za miundombinu ya barabara endelevu, huku utafiti ukilenga pia kuboresha uimara wa barabara na kukabiliana na changamoto za mazingira.
Changamoto ya barabara haiishii kwenye ubora wa lami. Maji ni miongoni mwa maadui wa miundombinu. Katika maeneo ambayo maji yako karibu na tabaka za barabara, uimara wa barabara unaweza kuwa changamoto kubwa.
Ndiyo maana teknolojia zinazolenga kuimarisha tabaka la barabara zinaweza kuwa na maana kubwa kwa Tanzania.
Dkt. Madirisha anasema bidhaa hizo zina uwezo wa kutoa uimara unaohitajika katika matumizi ya ujenzi na pia zina faida ya kutoshambuliwa kwa urahisi na chumvi.
Hapa ndipo ubunifu wa ndani unapokuwa na thamani ya kipekee.
Kwa sababu badala ya kusubiri teknolojia itoke nje ndipo Tanzania ianze kujiuliza kama inaweza kuendana na mazingira yake, watafiti wa ndani wanajaribu kutengeneza suluhisho kwa kuanzia kwenye changamoto zinazojulikana hapa nchini.
Habari Picha 13306
Anasema UDSM pia imebuni Bentox, bidhaa inayotumika kuziba nyufa na ambayo inaweza kutumika katika baadhi ya shughuli za viwandani.
Kuna pia Flax, inayolenga kuchuja biogas kwa kuondoa baadhi ya gesi zisizohitajika, ikiwemo carbon dioxide na hydrogen sulfide, ili kuboresha ubora wa biogas.
Hii inaonyesha picha kubwa zaidi ya utafiti huo, kutafuta teknolojia zinazogusa ujenzi, nishati, mazingira na matumizi ya rasilimali.
Na muhimu zaidi, watafiti hawatazami teknolojia kama kitu kinachopaswa kutegemea malighafi za kutoka nje pekee.
Anasema watafiti wanaangalia mnyororo mzima wa uchakataji kwa lengo la kutumia kwa kiwango kikubwa malighafi zinazopatikana Tanzania.
Hapo ndipo tunapoweza kuona fursa nyingine kubwa, utafiti unaweza kuwa mwanzo wa viwanda.
Tanzania sasa ina Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayoweka mazingira na ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi miongoni mwa nguzo zake muhimu.
Serikali pia inasisitiza utekelezaji wa Dira hiyo kwa kushirikisha sekta binafsi na wadau mbalimbali.
Kwa hiyo, ubunifu wa aina hii unapata maana zaidi ya kuwa bidhaa mpya.
Ni sehemu ya safari ya kujenga Tanzania inayotumia maarifa, sayansi na teknolojia kutatua changamoto zake.
Ulimwengu nao unaelekea kwenye miundombinu inayozingatia mazingira. Kwa Tanzania, hatua hiyo si anasa.
Ripoti ya Benki ya Dunia kuhusu Tanzania inaonya kuwa mabadiliko ya tabianchi yanaweza kuathiri ukuaji wa uchumi na kuongeza idadi ya watu walio katika hatari ya umaskini, huku ikiweka msisitizo katika uwekezaji wa miundombinu yenye ustahimilivu na uzalishaji mdogo wa hewa ukaa.
Kwa hiyo, teknolojia zinazolenga kujenga kwa ufanisi zaidi na kwa kuzingatia mazingira zinaweza kuwa sehemu ya majibu ya changamoto hiyo.
Hata hivyo, hapa ndipo simulizi ya ubunifu huu inakuwa ya kuvutia zaidi.
Tanzania ina watafiti. Ina vyuo. Ina mawazo. Ina teknolojia.
Lakini bado kuna swali moja,
Je, tunaweza kuufikisha ubunifu huo kwa mwananchi kwa kiwango kikubwa?
Dkt. Madirisha anasema uzalishaji wa bidhaa hizo bado ni mdogo, licha ya kuwepo kwa watu wanaozihitaji.
Changamoto kubwa ni ukosefu wa vifaa vya kisasa vya uzalishaji kwa kiwango kikubwa.
Anasema moja ya mashine zinazohitajika ni “flash cascade machine”, inayopatikana China kwa gharama inayokadiriwa kufikia dola 200,000 za Marekani.
“Tunamini tukipata mashine kama hii itaweza kutusaidia kutoka tulipo na kwenda kwenye uzalishaji mkubwa na hivyo kuweza kukidhi mahitaji ya wateja wanaohitaji bidhaa hizi,” anasema.
Hapa ndipo serikali, sekta binafsi, taasisi za utafiti na wawekezaji wanapopaswa kujiuliza, tunawezaje kuufanya ubunifu wa Tanzania uwe bidhaa ya Tanzania?
Dkt. Madirisha anatoa wito kwa wadau mbalimbali, wakiwemo Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Wizara ya Nishati, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kushirikiana na watafiti katika kukuza matumizi ya teknolojia hizo.
Wito huo una umuhimu mkubwa kwa sababu mafanikio ya utafiti hayapimwi kwa idadi ya karatasi zilizochapishwa pekee.
Mafanikio yake makubwa zaidi yanaonekana pale ambapo utafiti unabadilisha maisha.
Mtafiti akibuni teknolojia ya barabara, barabara ikawa imara zaidi; teknolojia ya nishati, wananchi wakapata nishati bora; teknolojia ya mazingira, uchafuzi ukapungua.
Hapo ndipo maarifa yanapogeuka kuwa maendeleo.
Ubunifu wa watafiti wa UDSM umeendelea kutambuliwa kupitia tuzo mbalimbali. Dkt. Madirisha anasema ubunifu huo umetambuliwa katika Wiki ya Utafiti na Ubunifu, huku mradi huo ukipata tuzo ya ubunifu wenye kuleta mabadiliko yenye zawadi ya Sh. Milioni 10 kutoka Kampuni ya Bahari.
Anasema mshindi wa mwaka alipata zawadi ya Sh. Milioni tano kutoka Benki ya CRDB.
Kwa upande wake, Dkt. Madirisha anasema pia ametambuliwa kutokana na mchango wake katika utafiti na uchapishaji wa machapisho ya kitaaluma katika majarida ya kimataifa.
Anasema alikuwa na machapisho matatu yaliyotambuliwa kutokana na ubora na athari yake katika utafiti.
Tuzo hizo ni ishara kwamba ubunifu wa Tanzania unaweza kutambuliwa.
Lakini tuzo pekee hazitoshi.
Kinachohitajika ni kuhakikisha teknolojia hizo zinapata mazingira ya kukua, kufanyiwa majaribio zaidi, kuzalishwa kwa wingi na hatimaye kutumika na wananchi.
Katika historia ya maendeleo, nchi hazijengwi na majengo na barabara pekee.
Nchi hujengwa na maarifa yanayobadilishwa kuwa suluhisho.
Novacem, Duracem na Duracem 1A zinatoa mfano wa kile kinachoweza kutokea pale utafiti unapounganishwa na mahitaji halisi ya jamii.
Ni mfano unaotukumbusha kwamba suluhisho la changamoto za Tanzania si lazima lianzie nje ya mipaka yake.
Linaweza kuanzia katika maabara ya chuo kikuu. Linaweza kuanzia kwa mtafiti anayekataa kukubali kuwa changamoto fulani haina jibu.
Na linaweza kuishia kwenye barabara ambayo mtoto anatumia kwenda shule, mkulima anayotumia kusafirisha mazao na mfanyabiashara anayotumia kufikisha bidhaa sokoni.
Ndiyo maana sasa kazi haipaswi kuishia kwa mtafiti. Serikali ina wajibu wa kuweka mazingira. Sekta binafsi ina wajibu wa kuwekeza. Vyuo vina wajibu wa kuendelea kutafiti. Na jamii ina wajibu wa kuamini na kutumia ubunifu wa ndani pale unapokidhi viwango.
Tanzania inaweza kuendelea kuagiza teknolojia kutoka nje, lakini inaweza pia kuanza kusafirisha teknolojia zake.
Na pengine, barabara imara zaidi ya Tanzania ya kesho inaweza kuwa inaanza leo si kwenye lami, bali ndani ya maabara za watafiti wake.
Habari Picha 13307

You Might Also Like

Tujenge Jumuiya Yenye Mustakabali wa Pamoja kati ya China na Afrika – Wang Yi

Warsha Ya Luban Yaleta Mapinduzi Ya Elimu Ya Ufundi Nchini Tanzania

Wanachuoni Katika Mawasilianao ya Utamaduni kati ya China na Afrika

Kenya, Tanzania Zashirikiana na China Kukabiliana na Changamoto za Ushuru wa Marekani

Kinywaji Cha China Chavuka Mipaka Chatua Tanzania

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mnyama Check App: Ubunifu Wamtoa Mfugaji Gizani hadi Kidijitali
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mnyama Check App: Ubunifu Wamtoa Mfugaji Gizani hadi Kidijitali
Makala August 18, 2026
Waziri Mkenda Kuzindua Wiki Ya Elimu,Ujuzi Na Ubunifu,Washiriki Takriban 300 Waonesha Bunifu Mbalimbali
Habari August 17, 2026
VETA Kibaha Yatengeneza Simu Ya Mkononi Yenye Uwezo Wa Kupiga Na Kutuma Sms
Habari August 17, 2026
Wiki Ya Elimu, Ujuzi Na Ubunifu,UDSM Yabuni Dema La Kidigitali La Milango Sita Kusaidia Wavuvi
Habari August 17, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

[mc4wp_form id=”2408″]

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?