Na Lucy Lyatuu,Dodoma
WAKALA wa Majenga Tanzania (TBA) umesema tayyari umeainisha maeneo kwa ajili ya uwekezaji na wanawaalika wawekezaji kushirikiana nao katika miradi ya pamoja katika maeneo hayo.
Ametaja maeneo yaliyoainishwa kuwa ni pamoja na Mwanza,Arusha,Dodoma,Meya,Dar es Saala na Songwe.
Ofisa Uhusiano wa TBA,Renatus Sona amesema hayo leo wakati akizungumza katika banda la TBA lililoko katika maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma inayofanyika katika viwanja vya Chingangali Park mkoani humo.

Kuhusu uwekezaji amesema wanatumia wiki ya utumishi wa umma kukaribisha wananchi na wawekezaji kushirikiana nao kutekelezw miradi mbalimbali .
Amesema katika banda hilo wapo wataalam mbalimbali wa ujenzi wanaotoa elimu kuhusu ujenzi wa majengo na taarifa zaidi zinazohusu miradi ya wakala huo.
Sona amesema katika maonesho hayo wana kauli mbiu ya kuchochea uwajibikaji jumuishi katika kutoa huduma endelevu ambayo inaakisi kazi zao wanazofanya,
” Tunasimamia miliki za serikali, tunajenga na kusimamia miradi katika ujenzi na katika kazi zote za ujenzi tunafanya kwa umoja kila mmoja ana umuhimu wake na ili jengo liweze kukamilika lazima liwe na mbunifu majengo,’ amesema na kuongeza kuwa sheria imefanyiwa marekebisho na sasa inaruhusu kufanya miradi kwa ubia.
Amesema katika ubia huo ni miradi kushirikiana na Wakala huo, sekta binafsi na taasisi za kifedha, hivyo wanakaribisha wananchi na hata wawekezaji ili kushirikiana katika miradi hiyo.
Ameongeza kuwa kwa Dodoma ipo miradi mikubwa waliyonayo ukiwepo mradi mkubwa wa nyumba 3500 za makzi kwa ajili ya watumishi wa umma ambao unatekelezwa katika eneo la Nzuguni B na unatekelezwa kwa awamu.
Amesema kwa awamu ya kwanza wameshajenga nyumba 150 ambazo zimekamilika na tayari watumishi wa umma wameingia na wanategemea kuzindua nyumba nyingine ambazo ziko katika hatua mbalimbali za kukamilika.

” Pia tunaendelea na ujenzi wa nyumba za serikali ,mradi ambao ni mkubwa ukiwa na ofisi mbalimbali za serikali ambao uko eneo la Mtumba,” amesema na kuongeza kuwa ipo miradi wanasimamia na kutoa ushauri ukiwemo wa Ruwasa ambao makao makuu yao yapo Njedengwa , mrari wa Tume ya madini na wa umwagiliaji.
Sona ametoa ushauri kwa wananchi kushiriki katika wiki hiyo kujifunza kuhusu namna ya kujenga nyumba bora na kwa gharama nafuu.

