Na Lucy Lyatuu, Dodoma
TAASISI ya Kudhibiti Ubora Wa Mbegu Tanzania (TOSCI) inawataka wakulima kuitumia taasisi hiyo kupata mafunzo ya kina kuhusu mbegu bora na namna ya kuzifahamu zile mbegu bandia.
Mtafiti Na Mkaguzi Wa Mbegu kutoka TOSCI, Neema Yohana amesema hayo katika banda la taasisi hiyo lililopo katika viwanja vya Chinangali Park kwenye Wiki ya Utumishi inayoendelea jijini Dodoma.
Amesem matumizi ya mbegu bandia yamesababisha wakulima kupote@ kipato kwa kupata mazao hafifu na hata kutopata mavuno kabisa.
” Sheria ya mbegu ya mwaka 2003 inamlinda mkulima asiuziwe mbegu zisizo na ubora ama mbegu bandia,” amesema Neema na kuongeza kuwa Taasisi hiyo inashiriki katika wiki hiyo kutoa elimu kwa wakulima,hivyo ni muhimu kufika ili kupata uelewa wa kutosha.
Amesema yapo mambo muhimumya kuzingatia wakati wa kununua mbegu ikiwa ni pamoja na kununua mbegu zilizoidhinishwa kupandwa katika ukanda uliopo,kununua mbegu iliyo kwenye kifungashio halisi ambacho hakijafunguliwa na chenye maelezo ya jina la kampuni, na fungu la mbeigu.
Amesema mambo mengine muhimu ni aina ya jamiimya zao,asilimia ya uotaji,asilimia ya usafi na tarehe ya kupimwa ubora maabara na kununua mbegu iliyo na lebo ya TOSCI.

