MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: JAB yawaonya wanaofanya kazi za kihabari bila ithibati
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > JAB yawaonya wanaofanya kazi za kihabari bila ithibati
Habari

JAB yawaonya wanaofanya kazi za kihabari bila ithibati

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: BODI ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imebaini kuwa baadhi ya watu wasio na sifa za kitaaluma wameanza tena kutekeleza majukumu ya kihabari baada ya kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu, Oktoba 29, 2025.
Akizungumza kuhusu hali hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Patrick Kipangula, amesema Bodi inawakumbusha wadau wote kuwa uandishi wa habari ni taaluma rasmi inayosimamiwa na misingi ya kisheria, maadili na weledi wa kitaaluma.
Amesisitiza kuwa mtu yeyote anayejihusisha na shughuli za kihabari bila kuwa na ithibati halali anakiuka masharti ya sheria.
Kipangula ameeleza kuwa makundi yanayotakiwa kuwa na ithibati ni pamoja na wahariri, waandishi wa habari, waandishi huru, wapiga picha za habari, wazalishaji wa vipindi pamoja na watangazaji wa redio na televisheni wanaofanya kazi katika vyombo vya habari.
“Kwa muktadha huo, Bodi inatoa onyo na kuwataka watu wote wanaotekeleza shughuli za kihabari bila kuwa na ithibati kuacha mara moja.
“Kuendelea kufanya hivyo ni kosa kisheria kwa mujibu wa Kifungu cha 50(2)(b) cha Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229,” amesema.
Ameongeza kuwa Bodi haitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu au taasisi yoyote itakayobainika kuajiri au kuruhusu utekelezaji wa kazi za kihabari bila kufuata utaratibu na masharti yaliyowekwa kisheria.
Vilevile, JAB imeutaarifu umma na wadau wa sekta ya habari kuwa katika kipindi cha hivi karibuni itaendesha ukaguzi maalum katika vyombo vya habari na maeneo mbalimbali nchini.
Ukaguzi huo unalenga kujiridhisha kuwa wanaotekeleza majukumu ya kihabari wanakidhi vigezo vinavyotakiwa kwa mujibu wa sheria.
Bodi imetoa wito kwa wote wenye nia ya kufanya kazi za kihabari kuhakikisha wanapata ithibati halali, wanazingatia maadili na weledi wa juu wa taaluma, na kutumia kalamu, sauti na majukwaa yao kuwahudumia wananchi kwa kutoa taarifa sahihi, kukuza uwajibikaji na kuchangia maendeleo endelevu ya Taifa.

You Might Also Like

Baraza la uuguzi na ukunga lawakaribisha wenye malalamiko

MOI Kuendesha Kambi Maalum Ya Uchunguzi,  Ushauri Wa Kitabibu Kwa Wazee

Umwagiliaji kumwezesha mkulima kulima mara mbili mpaka tatu kwa mwaka

NIT Yasema Ina Uwezo Wa Kufundisha Kozi Ya Urubani

RC Serukamba Aiunga Mkono REAUgawaji Wa Mitungi Ya Gesi Iringa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Vikao vya Kamati za Bunge Kuanza Januari 13, 2026 Dodoma
Next Article TEA, UNICEF Watekeleza Miradi ya Elimu Visawani Zanzibar
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TPDC Kufikisha Gesi Nchi Nzima  Ndani Ya Miaka Miwili Na Nusu  Kuanzia Sasa
Habari March 11, 2026
Nchimbi Ahimiza Ushirikiano wa Wizara Katika Uhifadhi wa Mazingira
Habari March 10, 2026
Mtaka, Ndunguru Wakubaliana Ujenzi wa Maabara ya Kimkakati Njombe
Habari March 10, 2026
Wataalamu wa Fedha SADC Wakutana Pretoria Kujadili Bajeti
Habari March 9, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?