MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TANESCO Kutambulisha Mfumo Wa Kufunga Nyaya Kwenye Nyumba Ukifuatilia Matumizi Ya Umeme
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TANESCO Kutambulisha Mfumo Wa Kufunga Nyaya Kwenye Nyumba Ukifuatilia Matumizi Ya Umeme
Habari

TANESCO Kutambulisha Mfumo Wa Kufunga Nyaya Kwenye Nyumba Ukifuatilia Matumizi Ya Umeme

Author
By Author
Share
4 Min Read
Na Lucy Lyatuu
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limetambulisha rasmi mfumo mpya wa kufunga nyaya kwenye nyumba  ambao utawezesha  kufuatilia matumizi ya nyumba ya umeme  kupitia simu ya mkononi mfumo ujulikanao  kama smart house.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange amesema hayo wakati akizungumzia mambo muhimu aliyomueleza Rais Wa Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi alipotembeleza banda hilo lililopo katika maonesho ya 50 ya biashara ya kimataifa maarufu kama Sabasaba.
Habari Picha 12843
Amesema kupitia mfumo huo, simu itakuonyesha chombo gani ndani ya nyumba kinatumia umeme zaidi kwa hiyo unaweza ukakizima  huko huko uliko.
“Hata kama uko Mwanza, Dubai nyumba iko kigoma unaweza uka switch off hicho kifaa ili matumizi yale unayoyahofia yakasimama,” amesema Twange na kuongeza kuwa ubunifu huo umetokana na Shirika kupata  malalamiko kadhaa kutoka kwa wateja kwamba  matumizi sio makubwa lakini umeme kuisha haraka.
Amesema malalamiko mengine ni  mita kutokusoma vizuri na kuwataka  TANESCO kwenda kufanya ukaguzi na mambo mengine,hivyo mfumo huo utatoa suluhu ya kujua chombo kinachotumia umeme mwingi ndani ya nyumba.
Amesema  hiyo ni teknolojia mpya ambapo wataizindua  muda si mrefu kuisambaza kwa wateja jamno linaloonesha kuwa  wahandisi wameumiza vichwa na ni jambo hilo liko mezani.
Habari Picha 12844
 Amewataka wateja  wa umeme kuendelea   kujua kwamba kila siku wanaumiza vichwa kadri wanavyopata changamoto kutoka kwao na wanaumiza vichwa vya kutafuta suluhu ya changamoto zao.
 Hata hivyo alimshukuru sana Rais  zanzibar Dkt Mwinyi  kupata muda wa kutembelea banda  la tanesco na kuona  mambo mengi wanayoyfanya.
 Amesema amemweleza Rais Dkt Mwinyi  hatua zinazochukuliwa na Shirika  juu ya kutekeleza mkakati wa nishati safi ya kupikia  na kwamba wameshapewa maelekezo ambapo wanatengeneza mbinu tofauti tofauti za kutekeleza
” kwa hiyo kwa sasa tuna mpango unaitwa ni bill financing ambao unaendelea hapo wateja wetu ambao ni wapya na wale ambao tayari wanatumia umeme wanaweza wakakopeshwa majiko na wakawa wanalipa mkopo wao kadri wanavyonunua umeme,” amesema.
Amesema  mpango umekuwa na mwitikio mzuri  wa mafanikio zaidi ya asilimia  90 kwa hiyo umefanikiwa na ndio maana  wameingia kwa sekta binafsi ambao wako nao kama wadau.
“Tumesaini nao mikataba na tumeanza kazi ya kukopesha majiko haya kwa wananchi kwa hiyo naendelea kutoa wito kwa wananchi wote wasiogope kutumia umeme tayari wenzao wameshaonyesha njia hii ndio nishati nafuu zaidi kuliko nishati zingine,” amesema na kuongeza kuwa wanasayansi na wahandisi wameshatengeneza majiko ambayo yanatumia umeme rafiki na utafurahi ukilinganisha na gharama unazitumia kutumia nishati nishati nyingine.
Habari Picha 12845
Aidha amesema amemueleza Rais Dkt Mwinyi kuhusu utekelezaji wa mradi mkubwa wa kujenga njia mpya za kusafirisha umeme kutoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar.
 Amesema katika mradi huo utakuwa na njia za umeme tatu za kupita chini ya maji  ikiwa  inatoka Dar es Salaam kwenda Unguja kutoka Tanga kwenda Pemba na ya kwenda Mafia.
Amesema  ule ni mradi mhandisi mshauri atapatikana Agosti na wanatarajia kumpata mkandarasi Januari na muda wa utekelezaji  ni miezi 20, 22.
Twamge amesema  mradi kukamilika kwake utaongeza uwezo wa  kupeleka umeme  mwingi zaidi zanzibar ambayo  imejengwa sana katika kipindi cha miaka mitano ya Rais Dkt Mwinyi.

You Might Also Like

Serikali Yaendelea Kuimarisha Sekta Ya Utalii, Mapato Yaongezeka

Marekebisho ya sheria huangalia mazingira ya sasa na yajayo – Tume

Trump Amteua Mtendaji Mkuu White House, Safari Ya Kuunda Timu Yake

TPHPA Yaimarisha Mapambano Dhidi Ya Visumbufu Vya Mazao

Wajumbe TSC watakiwa kutembelea ofisi ngazi ya wilaya

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Wananchi Waendelea Kunufaika Na Ofa Za TTCL Sabasaba 2026
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Wananchi Waendelea Kunufaika Na Ofa Za TTCL Sabasaba 2026
Habari July 13, 2026
Ruhuka: Mdudu Anayetishia Zao la Kahawa, TARI Yaja na Suluhisho
Habari July 12, 2026
BRELA Yaja Na Mfumo BOS Uliounganisha Mifumo Yote
Habari July 12, 2026
Misitu Ni Moyo Wa Maendeleo Endelevu-TFS
Habari July 12, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?