Na Lucy Lyatuu,Dodoma
WIZARA ya Katiba Na Sheria imetatua kesi 100 ambazo ni changamoto kutoka kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo zinazohusu ardhi, mirathi, utapeli na ubabe.
Waziri wa Katiba Na Sheria, Juma Homera amesema hayo wakati akisikiliza kero za wananchi chini ya kipindi cha nne cha Sema na Waziri na kwamba utaratibu wa kusikiliza wananchi utaendelea kufanyika mara tatu kwa mwezi.
Akizungumza, Homera amesema wananchi wengi wamekuwa wakionewa na kuwataka kuendelea kupiga simu kueleza malalamiko yanayowasibu ili waweze kupata unafuu wa maisha na kupata haki zao.
” Wananchi hawana ulazima wa kwenda mahakamani…kipindi cha Sema na Waziri ni fursa kwao kujinga na kuzungumza moja kwa moja na kiongozi wao ili kusaidiwa,” alisema Waziri Homera na kuongera kuwa simu zaidi ya 30 zimepokelewa katika kipindi hicho.
Amesema kipindi hicho kimekuwa kikisaidia wananchi na hio ni kutokana na wananchi wengi kushindwa kujua sehemunya kuzifikisha changamoto zinazowakabili hivyo wajue wanaweza kunufaika na Wizara yao na kuondoa ukiritimba kwa wanaoonea wengine.
Ametaja miongoni mwa kesi zilizosikilizwa na kufanyiwa kazi kuwa ni pamoja na ile ya mwanamke aliyekuwa akifanyiwa vitendo vya ukatili kwa kupigwa na mume wake ambapo wizara imefuatilia na kumchukulia sheria mwanaume huyo na kuchukuliwa hatua.
Homera ametaja kesi nyingine kuwa ni inayohusu mzabuni aliyejenga shule katika halmashauri ya Nzega Tabora ambapo alikuwa akiidai Halmashauri hiyo fedha kwa muda mrefu bila mafanikio ambapo Waziri ameweza kuzungumza na Mkurugenzi moja kwa moja na kuahidi kufuatilia suala hilo na kumlipa mlalamikaji.
Shauri lingine ni la mwanafunzi wa Taaisi yanTeknolojia tawila Mwanza ( DIT ),Mwanza ambapo alidahiliwa katika kozi ya uhandisi lakini akapelekwa kozi nyingine ya kilimo lakini baada ya Waziri kusikiliza shauri hilo amehakikisha amerudishwa katika emfumo husika.
Homera amesema lipo shauri la mmiliki wa kiwanja namba 35 block A eneo la Mchechere Mwanza ambapo mmiliki amenyanga’anywa umiliki na hati yake kupewa mtu mwingine,ambapo ameahidi kupeleka timu yake ya wanasheria katika mkoa huo akishirikiana na Mkuu wa mkoa huo ili kufikia muafaka.
Amesema mbali na shauri hilo wapo wananchi wengi wenye malalamiko kama hayo na hiyo ikionesha kuna uonevu mwinginunaofanyika kwa wananchi wengine wakitumia ubabe wa fedha kuumiza wengine na kwa kupitia kipindi hicho atahakikisha wananchi wanapatiwa haki zinazowastahili.

