MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Majaliwa Asisitiza Serikali Itaendelea Kuboresha Mazingira Ya Uwekezaji
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Majaliwa Asisitiza Serikali Itaendelea Kuboresha Mazingira Ya Uwekezaji
Habari

Majaliwa Asisitiza Serikali Itaendelea Kuboresha Mazingira Ya Uwekezaji

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali itaendelea kufanya maboresho zaidi ya mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuifanya Tanzania iwe sehemu salama zaidi ya uwekezaji.
Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Aprili 3, 2025 wakati wa uzinduzi wa Maandalizi ya Mpango wa Pili wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini (MKUMBI II) katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Amesema kupitia mpango ambao ameuzindua, maandalizi yake pamoja na kamati zake, Serikali itaweza kushughulikia mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kiteknolojia ili kuweka mazingira bora zaidi kwa wafanyabiashara na wawekezaji.
“Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa wadau wote ili kufanikisha malengo ya kuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara.
“Ni mategemeo yetu kuwa, mpango huu utaongeza tija kubwa kwa Taifa letu na kusaidia kufikia malengo yetu ya kuwa na uchumi wa kati ulio endelevu,” amesema.
Ameelezea umuhimu wa MKUMBI II, ni pamoja na kuvutia wawekezaji wa nje na ndani, kuongeza fursa za ajira, kuboresha miundombinu, upatikanaji wa soko la kimataifa kwa bidhaa za ndani, kukuza ushindani na ubora wa bidhaa.
Ameisisiti kamati ya maandalizi ya MKUMBI II iharakishe maandalizi ya mpango huo ili utekelezaji wake uweze kuanza mara moja na kurahisisha mazingira bora kwa wafanyabiashara na wawekezaji.
Amezitaka Taasisi na Mamlaka za Udhibiti za Serikali ambazo zitahusishwa katika utafiti na tathmini zitoe ushirikiano wa dhati kwa kamati ili iweze kuja na mapendekezo mahsusi yenye malengo mapana ya nchi ambayo yataendana na Dira ya Taifa 2050.
Kwa upande wake, Waziri Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema lengo la Serikali la kuandaa mpango huo ni kuona Tanzania inakuwa sehemu bora na ya kuvutia ya kufanya biashara na uwekezaji.
“Kazi ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ni kazi endelevu,” amesema.
Amesema ili uchumi uweze kukua ni lazima mazingira ya biashara na uwekezaji yafanyiwe mapitio na maboresho ya mara kwa mara, na ndio maana kamati ya kitaifa ya wataalam iliyoundwa imezingatia matakwa ya sasa ya uhitaji wa biashara na uwekezaji.

You Might Also Like

Wananchi Washauriwa Kujiunga Na Chuo Cha Ualimu Na Ufundi Stadi Morogoro

TPHPA Yapata Tuzo ya WCO kwa Ulinzi wa Afya na Usalama wa Taifa

October 2, 2024

Rais Samia Amehakikisha Elimu Ya Ufundi Stadi Inafikia Vijana Wote – Mkenda

Wizara Ya Elimu Yaomba Kuidhinishiwa Trilioni 2.3

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article REA Yapamba Moto Uhamasishaji Matumizi Ya Umeme
Next Article Maofisa Habari Watoe Taarifa Sahihi Ziwafikie Wananchi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Hananja Awataka Vijana Kufikiri Mara Mbili Kabla ya Kufuata Wito wa Maandamano
Habari June 18, 2026
June 18, 2026
Habari June 18, 2026
Magereza Yaomba Jamii Kuwapokea Wafungwa Wanaorejea Kutumikia Taifa
Habari June 18, 2026
TPHPA Yasisitiza Matumizi Sahihi ya Viuatilifu kwa Wakulima
Habari June 18, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?