MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wizara ya Maji Yawasilisha Vipaumbele 2026/2027 kwa Bajeti ya Trilioni 1.2
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wizara ya Maji Yawasilisha Vipaumbele 2026/2027 kwa Bajeti ya Trilioni 1.2
Habari

Wizara ya Maji Yawasilisha Vipaumbele 2026/2027 kwa Bajeti ya Trilioni 1.2

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso, amewasilisha bajeti ya takriban Sh. Trilioni 1.2 kwa mwaka wa fedha 2026/2027, akieleza vipaumbele vitakavyoimarisha upatikanaji wa majisafi na salama kwa Watanzania.
 Akiwasilisha hotuba hiyo Bungeni jijini Dodoma, amesema Serikali itaendelea kuimarisha usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji ili kuhakikisha usalama na upatikanaji wake kwa matumizi ya kijamii, kiuchumi na kimazingira.
Katika mwaka huo wa fedha, Wizara itakamilisha maandalizi ya Mpango Kabambe wa Taifa wa Maji pamoja na kuendeleza utekelezaji wa miradi ya Gridi ya Taifa ya Maji, inayolenga kusambaza maji kutoka vyanzo vya uhakika kama mito na maziwa kwenda maeneo yenye uhaba mkubwa.
Habari Picha 11975
Pia, Wizara itaongeza juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuimarisha uvunaji na uhifadhi wa maji ya mvua.
Mpango uliopo unahusisha ujenzi na ukarabati wa mabwawa 33, ubunifu wa mabwawa mapya 34, pamoja na tathmini ya athari za kimazingira kwa mabwawa mawili.
Wananchi pia watahamasishwa kuvuna maji ya mvua kupitia mapaa ya nyumba zao.
Katika kuboresha huduma, Wizara imepanga kukamilisha miradi 992 ya majisafi vijijini, miradi 196 mijini na miradi 26 ya usafi wa mazingira. Aidha, utekelezaji wa miradi mipya utaanza katika vijiji 314 kati ya 1,575 ambavyo bado havijafikiwa na huduma ya maji.
Waziri Aweso pia amesisitiza kudhibiti upotevu wa maji kwa kutumia teknolojia za kisasa kama mita za kielektroniki, mifumo ya usimamizi wa mtandao wa maji, na mita za malipo ya kabla. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya waharibifu wa miundombinu na wanaojihusisha na wizi wa maji.
Kipaumbele kingine ni kuhakikisha shule na vituo vya afya vinapata huduma ya maji na usafi wa mazingira.
 Wizara itashirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo TAMISEMI kufanikisha azma hiyo.
Ili kufanikisha mipango hiyo, Wizara itatumia vyanzo mbadala vya fedha kama hati fungani, ushiriki wa sekta binafsi na fedha za mabadiliko ya tabianchi.
Pia itaendelea kuimarisha TEHAMA, rasilimali watu, pamoja na mifumo ya ufuatiliaji na tathmini ya miradi.
Bajeti hii inalenga kuharakisha upatikanaji wa majisafi na salama kwa wananchi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kukuza ustawi wa jamii na uchumi wa taifa.

You Might Also Like

Walimu Wanaofundisha Lugha Ya Kichina Tanzania Wakutana

VETA Dodoma Waleta Mashine Kurahisishia Upekechuaji Wa Alzeti

Waratibu Wa Kitaifa Wa Nchi Za Jumuiya Ya Ukanda Wa Maziwa Makuu Wakutana Kinshasa

Majaliwa: Jiungeni NHIF Kupata Matibabu Ya Uhakika

Samia Mgeni Rasmi Siku Ya Mashujaa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article CCM  Yapokea Mapendekezo Ya Tume Ya Kuchunguza Vurugu Za Uchaguzi Oktoba 25,2025
Next Article Waziri Aweso Aainisha Mikakati ya Kuboresha Huduma ya Maji
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Waziri Aweso Aainisha Mikakati ya Kuboresha Huduma ya Maji
Uncategorized May 5, 2026
CCM  Yapokea Mapendekezo Ya Tume Ya Kuchunguza Vurugu Za Uchaguzi Oktoba 25,2025
Habari May 5, 2026
Mitandao Ya Kijamii Ilinde Maadili Ya Kitanzania-Makonda
Habari May 4, 2026
Rais Samia Amkabidhi Tuzo Profesa Ndunguru kwa Kuinua Mapato, Maboresho TPHPA
Habari May 3, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?