MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Malecela: Nitakuza Vipaji, Nitafutia Vijana Ajira Dodoma Mjini
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Malecela: Nitakuza Vipaji, Nitafutia Vijana Ajira Dodoma Mjini
Habari

Malecela: Nitakuza Vipaji, Nitafutia Vijana Ajira Dodoma Mjini

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Danson Kaijage
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini kupitia CCM, Samwel Malecela, ameahidi atatoa kipaumbele kwa vijana kwa kuanzisha shule maalum ya kuibua vipaji kuanzia utotoni.
 Akizungumza na wajumbe wa CCM katika Kata ya Mpunguzi, Malecela amesema vipaji vimekuwa chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana duniani kote, hivyo kuvitambua na kuviendeleza mapema ni njia sahihi ya kuwawezesha kiuchumi.
Amesema shule hiyo itakuwa kichocheo cha kuongeza kipato kwa vijana na kuchangia pato la jimbo zima.
“Leo hii vipaji ni ajira, na iwapo watoto wetu wataandaliwa mapema, watakuwa na nafasi kubwa ya kufanikiwa kuliko kusubiri hadi mtu awe mtu mzima,” amesema.
Sambamba na hilo, ameahidi kushughulikia upatikanaji wa mikopo ya halmashauri kwa wakati kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Amesema akiwa mbunge, atatumia nafasi yake kushinikiza utoaji wa mikopo hiyo usicheleweshwe, kwani ni haki yao kwa mujibu wa sera za serikali.
Aidha, Malecela alizungumzia mpango wa kuvutia wawekezaji hasa katika kata ya Matumbulu, ili kuongeza ajira na kukuza uchumi wa maeneo hayo.
Amesema pia changamoto ya maji kama moja ya kipaumbele atakachoshughulikia kwa kushirikiana na serikali kupitia utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Vile vile amesema Katika kata ya Mkonze, Samwel Malecela amekemea vikali vitendo vya upotevu wa mali za umma na migogoro ya ardhi vinavyoathiri maendeleo ya wananchi.
Akijibu maswali ya wajumbe wa CCM katika kata hiyo, amesema hatakubali wananchi kuendelea kunyimwa maendeleo kwa sababu ya ubadhirifu wa wachache.
“Baadhi ya watumishi wamekuwa wakihusika na ufisadi wa mali za umma huku wananchi wakibaki masikini.
“Hili ni jambo nitakalokomesha nikiwa mbunge,” amesema.
Pia aliahidi kushughulikia kero ya barabara kwa kuhakikisha zinajengwa kwa kiwango cha changarawe ili ziweze kupitika kwa urahisi.

You Might Also Like

Boti yazama abiria 14 kati ya 21 waokolewa

TPHPA Kuipokea Ndege Yake

Tigo yawafikia wakulima, wafugaji. Wavuvi nanenane Dodoma

Tanzania Kuweka Muongozo wa Kitaifa wa Usimamizi wa Takwimu Kidijitali

Mvua, Upepo Yaharibu Shule Lindi, Serikali Yatoa Milioni 96

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Njaa, Mafao Ya Wakulima Vyatikisa Kampeni Za Ubunge Dodoma Mjini
Next Article Rais Samia Aipa Neema Miradi Ya Kuzalisha Umeme Iringa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Teknolojia Ya Juisi YA Ndizi Kali Yafungua Fursa Mpya Za Viwanda, Ajira
Makala Uncategorized June 12, 2026
Serikali Yaingia Makubaliano Ya Ushirikiano Na DIT Kuimarisha Usimamizi Wa Mataifa
Habari June 8, 2026
Wananchi Waelimishwa Masharti ya Kubadilisha Noti Zilizochakaa, Kuungua na Kuchanika
Habari June 7, 2026
DMI Yawaalika Vijana Kujiunga Na Masomo Ya Ubaharia
Habari June 6, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?