MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Waziri Nanauka Aipongeza   TARURA Kwa Mpango Wa  CBRM ‎
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Waziri Nanauka Aipongeza   TARURA Kwa Mpango Wa  CBRM ‎
Habari

Waziri Nanauka Aipongeza   TARURA Kwa Mpango Wa  CBRM ‎

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Lyatuu,Dodoma
‎WAZIRI wa Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana,  Joel  Nanauka ameipongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa utekelezaji wa Mpango wa Matengenezo ya Barabara kwa Kutumia Vikundi vya Kijamii (CBRM) akieleza kuwa ni fursa muhimu ya kuwawezesha wananchi hususan vijana kushiriki katika shughuli za matengenezo ya barabara na kujiongezea kipato.
‎
‎Nanauka ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la TARURA katika Maonesho ya Kitaifa na Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayoendelea katika uwanja wa Dkt. John Malecela mkoani Dodoma.
‎
‎Amesema kuna umuhimu wa kuwafikia wananchi kwa kuwapa elimu ya kutosha kuhusu fursa zinazotolewa kupitia mpango wa CBRM ili waweze kushiriki kikamilifu. Aidha, amependekeza kuwepo kwa ushirikiano wa karibu kati ya Wizara ya Maendeleo ya Vijana na TARURA katika utekelezaji wa mpango huo.
‎
‎”Ni muhimu kuongeza kasi ya utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu fursa zilizopo katika mpango wa CBRM. Pia napendekeza kuwepo kwa vikao vya mara kwa mara kati ya Wizara ya Maendeleo ya Vijana na TARURA ili kuimarisha ushirikiano na kuhakikisha malengo ya mpango huu yanafikiwa”, amesema Nanauka.
‎
‎Kwa upande wake, Mratibu wa mpango wa CBRM TARURA Makao Makuu,  Richard Missa amemueleza Waziri huyo kuwa Wakala umeanza utekelezaji katika mkoa wa Tanga, Morogoro,Dodoma na Pwani ambapo barabara zaidi ya kilomita 1500 zinahudumiwa na vikundi 302 kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Habari Picha 13159
‎
‎Aidha, amesema Wakala umejipanga kutekeleza mpango wa CBRM katika mikoa yote 25 ya Tanzania Bara kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ambapo zaidi ya kilomita 7000 za barabara zitafanyiwa matengenezo na vikundi 1100 vitapata fursa katika kazi hizo.
‎
‎ Missa amesema mpango huo unalenga kuongeza ushiriki wa wananchi katika matengenezo ya kawaida ya barabara sambamba na kuchochea ajira na maendeleo ya kiuchumi katika jamii.
‎
‎TARURA itaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu utekelezaji na mafanikio ya mpango wa CBRM ili wananchi waendelee kunufaika na fursa zinazotokana na mpango huo.
‎
‎Wakati huo huo, TARURA imewahimiza wananchi kuendelea kutembelea banda lake katika Maonesho ya Nanenane ili kupata elimu kuhusu majukumu ya Wakala, ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu miundombinu ya barabara pamoja na kujionea mafanikio ya miradi inayotekelezwa nchini kwa lengo la kuimarisha maendeleo endelevu.

You Might Also Like

Kamati YA Siasa Yaendelea Kukagua Miradi Ya Maendeleo Temeke

TOSCI Inatoa Elimu Ya Kufahamu Mbegu Bandia

Samia, Nchimbi Kuchukua Fomu Ya Urais Kesho

Katibu Mkuu Uchukuzi Aipongeza TASAC,  Kuelimisha Wananchi 

Nchimbi Agongelea Nyundo Kwa Wagombea Watoa Rushwa

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article PURA Yawataka Watanzania Kujenga Uwezo Kunufaika Na Sekta Ya Mafuta Na Gesi
Next Article DC Kondoa  Aipongeza TFS Kwa Teknolojia Ya Uhifadhi Wa Misitu Na Utali
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

DC Kondoa  Aipongeza TFS Kwa Teknolojia Ya Uhifadhi Wa Misitu Na Utali
Habari August 8, 2026
PURA Yawataka Watanzania Kujenga Uwezo Kunufaika Na Sekta Ya Mafuta Na Gesi
Habari August 8, 2026
COSTECH Yapambania Haki Za Wabunifu, Yalenga Kupeleka Bunifu Sokoni
Habari August 8, 2026
Miaka 40 ya Costech: Ruzuku ya Ubunifu Imegeuza Wazo Kuwa Kiwanda Cha Kimataifa
Makala August 7, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?