Na Lucy Lyatuu, Morogoro
USHIRIKI wa Mamlaka Ya Elimu Na Mafunzo Ya Ufundi Stad (VETA) katika tamasha la nne la Utamaduni umekuwa na mafanikio makubwa hususani kwenye eneo la mavazi ambayo yamebuniwa kwa mitindo mbalimbali yenye kuimarisha utamaduni.
Meneja wa VETA Kanda ya Mashariki, John Mwanja amesema hayo katika kilele cha tamasha la nne la kitaifa la utamaduni lililofanyika mkoanj Morogoro kwenye uwanja wa Jamhuri.
Amesema mafanikio hayo yamefikiwa haswa baada ya uwekezaji wa vifaa vya kisasa vya ushonaji uliofanywa katika vyuo vya VETA Kanda ya Mashariki na kurahisisha maandalizi mazuri na mitindo mbalimbalu yenye ubunifu ambao umetumika katika tamasha hilo la utamaduni.


Ameongeza kuwa katika vyuo vilivyopo kwenye Kanda hiyo ambavyo ni vya Dakawa,Mikumi,Pwani na Kihonda wamenufaika na sh milioni 89.1 kwa ajili ya uwekezaji mkubwa ambao uliwezesha kununua vifaa vya kisasa vya fani ya ushonaji na kurahisisha ushonaji wa mavazi ambayo pia yalihumika kahika maonesho kwenye tamasha hilo.
“Tumeshiriki katika tamasha hili tukijikita zaidi katika maeneo mawili ya nguo za utamaduni ambazo zilishonwa katika vyuo vyetu lakininpia tumeonesha utalii wa kiutamaduni ambao ulihusisha ngoma,vyakula vya asili,nguo za asili ambazo zinaonesha asilinya Mtanzania,”amesema.
Aidha Mwanja amesema VETA katika ukanda huo kuna vyuo saba na kwamba vingine saba viko kwenye hatua ya kukamilishwa na kufikia mwakani inatarajiwa kuwa na vyuo 14 .

Amesema VETA inajivunia kushiriki kwa mara ya kwanza kwenye tamasha hususani katika eneo la utamaduni na kwamba wameona ni namna gani mafunzo watoayo yanavyoweza kuimarishwa ili kujibu eneo la utamaduni.
“Mara nyingi tulijielekeza kwenye ujuzi na ufundi lakini utamaduni na sanaa ilikuwa bado lakini baada ya Mamlaka kuanzisha mitaala.mbalimbali inazungumzia utamaduni na sanaa na michezo ,” amesema na kuwashauri vijana kujinga na VETA ili kujifunza eneo la utamaduni.


