Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 6, 2026
Habari Lucy Ngowi 7

Watumishi Wanawake Wa TEA wajitoa Kwa Jamii

Na Mwandishi Wetu
DODOMA: WATUMISHI wanawake wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA),  Leo Machi saba, 2025 wametembelea Kituo cha Kulea Watoto Miuji Nyumba ya Matumaini Jijini Dodoma kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani ambayo kilele chake huadhimishwa  Machi nane kila mwaka.
Katika ziara hiyo, wametoa msaada wa bidhaa mbalimbali, ikiwemo chakula vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 1.7 kwa ajili ya watoto 65 wanaolelewa kituoni hapo.
Mlezi wa kituo hicho,  Sr. Hellen akipokea msaada huo  ameishukuru mamlaka hiyo kwa mchango wao.
Akitoa shukrani hizo amesema, kituo hicho hutegemea misaada ya wadau ili kuhudumia watoto wake.
Naye Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala wa TEA, Alice Lukindo, amesema  wanawake wa TEA wameamua kusherehekea siku hiyo kwa kuleta faraja kwa watoto.
“Wanawake tuna wajibu wa kutunza familia na jamii. Leo tumeamua  kugusa maisha ya watoto hawa.”
“Kuadhimisha ni kufanya matendo mema,” amesema.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.