Na Lucy Lyatuu,Dodoma
TUME Ya Ulinzi Wa Taarifa Binafsi (PDPC) imetoa siku saba kwa taasisi ambazo zinakusanya na kuchakata taarifa binafsi na hazijakamilisha usajili kukamilisha kazi hiyo kuanzia Juni 12,2026.
Aidha imesema taasisi ambazo hazijaanza kabisa usajili zinatakiwa kuanza na kukamilisha ndani ya sikumsaba za kazi kuanziamJuni 12,2026.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Dkt Emmanuel Mkilia amesema hayo jijini hapa wakati akielezea kuhusu utekelezaji na uzingatiaji wa sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi sura ya 44 na kuongeza kuwa taasisi zote zinatakiwa kujiandaa kwa ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria ambao umekwishaanza na unaendelea.


Amesema taaasisi zote zinapaswa kuhakikisha zina sera zilizoidhinishwa za ulinzi wa taarifa binafsi na mifumo madhubuti ya ulinzi wa taarifa.
Amesema Tume imebaini kuwepo kwa taasisi zinazoendelea kukusanya na kuchakata taarifa binafsi bila kuzingatia matakwa ya sheria,hususani katika sekta nyeti kama afya na elimu.
Amesema hali hiyo ni ukiukwaji wa moja kwa moja wa sheria na inaleta hatari kwa hakimza msingi za faragha za wananchi na kwamba inawakumbusha wananchi kuwa wana haki ya kulinda taarifa zao binafsi kwa mujibu wa sheria.
“Wananchi wanahimizwa kutumia haki zao ikiwemo kuwasilisha malalamiko Tume endapo watabaini matumizi yasiyo halali ya taarifa zao au ukiukwaji wa faragha zao,” amesema na kuongeza kuwa Tume itaendalea kutoa elimu miongozo na usimamizi ili kuhakikishamTanzania inakuwa na mfumo imara wa ulin> wa taarifa binafsi u zolinda haki za wananchi na kuimarisha imani katika matumizi ya teknolojia na huduma za kidigitali.

Hata hivyo amesema Tume imepanga kufanya kongamano la kwanza la faragha na ulinzi wa taarifa binafsi kuanzia Juni 29 hadi Judi 1,202_ jijini Dar es Salaam.

