MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Ndejembi Ashuhudia Utiaji Saini Wa Mkataba Wa Sh Bilioni 204.7 Wa Mradi Wa Umeme Wa Jua Wa Megawati 100 Kishapu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Ndejembi Ashuhudia Utiaji Saini Wa Mkataba Wa Sh Bilioni 204.7 Wa Mradi Wa Umeme Wa Jua Wa Megawati 100 Kishapu
Habari

Ndejembi Ashuhudia Utiaji Saini Wa Mkataba Wa Sh Bilioni 204.7 Wa Mradi Wa Umeme Wa Jua Wa Megawati 100 Kishapu

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi ameshuhudia utiaji saini wa mkataba wa utekelezaji wa awamu ya pili ya Mradi wa Umeme wa Jua wa Kishapu wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 100, utakaotekelezwa katika eneo la Ngunga, Wilaya ya Kishapu, Mkoa wa Shinyanga.

Mkataba huo wenye thamani ya sh bilioni 204.7 umesainiwa leo kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na mwakilishi wa mkandarasi anayetekeleza mradi huo, kampuni za Sagemcom Energy & Telecom SAS na STEG International Services.

Habari Picha 12902

Waziri Ndejembi amesema mradi wa Umeme wa Jua wa Kishapu ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuimarisha mseto wa vyanzo vya uzalishaji wa umeme ikiwa ni utekelezaji wa azma ya kuongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika, wa gharama nafuu na unaotokana na vyanzo vya nishati jadidifu.

Amefafanua kuwa, mradi huo unatekelezwa kwa awamu mbili zenye uwezo wa jumla wa kuzalisha Megawati 150. Awamu ya kwanza yenye uwezo wa Megawati 50 iligharimu sh bilioni 118.3 na kwa sasa ipo katika hatua za mwisho za utekelezaji.

Aidha, Waziri Ndejembi amesema awamu ya pili yenye uwezo wa Megawati 100, ambayo utekelezaji wake umeanza rasmi kupitia utiaji saini wa mkataba utagharimu sh bilioni 204.7. Jumla ya gharama za utekelezaji wa awamu zote mbili ni shilingi bilioni 323.

Habari Picha 12903

Utekelezaji wa mradi huu unatarajiwa kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka vyanzo vya nishati jadidifu, kuimarisha uthabiti wa mfumo wa umeme nchini na kuchangia kufikiwa kwa lengo la Serikali la kuwa na mseto wa vyanzo vya uzalishaji wa umeme pamoja na kufikia uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye.

Hafla hii imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba; Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita; Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Felchesmi Mramba Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Subira Mgalu, pamoja na viongozi wengine wa Serikali, Chama cha Mapinduzi na wadau wa sekta ya nishati.

Habari Picha 12904

You Might Also Like

Samia Mgeni Rasmi Siku Ya Mashujaa

Askofu Akemea Midoli Kuvishwa Nguo Za Ndani

NIC Yaimarisha Uhusiano na Wateja Maonesho ya Teknolojia ya Madini Geita

June 18, 2026

Mbunge Aibana Serikali Kuhusu Malipo ya Wafanyakazi wa Zamani SPM Mgololo

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kutoka Wazo Rahisi Hadi Mapinduzi ya Kilimo: Safari ya Rafiki Planter Inayosimulia Miaka 40 ya COSTECH
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Kutoka Wazo Rahisi Hadi Mapinduzi ya Kilimo: Safari ya Rafiki Planter Inayosimulia Miaka 40 ya COSTECH
Makala July 27, 2026
Watendaji Wakuu Waagizwa Kuifanya Dira 2050 Kuwa Mwongozo Wa Maamuzi Yao
Habari July 24, 2026
Nchi za SADC Zahimizwa Kuimarisha Umoja Kukabili Changamoto
Uncategorized July 17, 2026
Wananchi Washauriwa Kutumia  Wataalam Wa Ujenzi Kuepuka Madhara
Habari July 14, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?