MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TEA, Wizara ya Elimu Zanzibar Kushirikiana Kuimarisha Miradi ya Elimu
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TEA, Wizara ya Elimu Zanzibar Kushirikiana Kuimarisha Miradi ya Elimu
Habari

TEA, Wizara ya Elimu Zanzibar Kushirikiana Kuimarisha Miradi ya Elimu

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Naibu Katibu Mkuu (Taaluma) Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Mwanakhamis Ameir (kulia) na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Kipesha (kushoto) wakisaini mkataba maalum kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya elimu visiwani Unguja na Pemba.
Na Mwandishi Wetu
ZANZIBAR: MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar zimesaini mkataba maalum wa kushirikiana katika utekelezaji wa miradi ya elimu itakayohusisha ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia katika shule 20 za sekondari visiwani Unguja na Pemba.
Hafla ya utiaji saini imefanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mazizini, Unguja ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu (Taaluma) Dkt. Mwanakhamis Ameir na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania Dkt. Erasmus Kipesha.
Habari Picha 11895

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Dkt. Erasmus Kipesha akisaini mkataba maalum wa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya elimu visiwani Unguja na Pemba.

Akizungumza mara baada ya kusainiwa kwa mkataba huo Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Dkt. Erasmus Kipesha amesema, jukumu kuu la mamlaka hiyo ni kutafuta rasilimali fedha na vifaa kutoka kwa wadau wa maendeleo ya sekta ya elimu ili kuboresha miundombinu ya elimu nchini.
Amebainisha kuwa tayari fedha zimepatikana kupitia wadau hao akiwemo UNICEF na kusisitiza umuhimu wa usimamizi madhubuti wa miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.
“Fedha tayari zipo kutoka kwa wadau wetu, hivyo ni wajibu wenu kuhakikisha miradi hii inatekelezwa ipasavyo na kukamilika kwa wakati,” amesema Dkt. Kipesha.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu (Taaluma) wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Mwanakhamis Ameir, ameishukuru TEA kwa kuendelea kuwekeza katika kuboresha miundombinu ya elimu visiwani humo.
Amesema licha ya juhudi zinazofanywa na Serikali, bado kuna changamoto kubwa katika sekta hiyo hivyo ushirikiano huo ni muhimu katika kuzitatua.
Dkt. Ameir amesisitiza kuwa, wizara iko tayari kuanza utekelezaji wa miradi hiyo mara moja huku akiwataka wataalamu wote wanaohusika kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha miradi haikwamishwi.
“Ni muhimu kuthamini ushirikiano huu na kuhakikisha thamani ya fedha inayowekezwa inaonekana kupitia utekelezaji bora wa miradi,” ameongeza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa awali na Mkurugenzi wa Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi ya Elimu Masozi Nyirenda, TEA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya uboreshaji wa miundombinu ya elimu katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Awali, takribani Sh. Bilioni 3.2 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule za amali, huku Bilioni 2.5 zikielekezwa katika ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo na maabara za sayansi katika shule 20.

You Might Also Like

Mwalunenge Kuunganisha Mbeya Mjini, Kusukuma Maendeleo Na Ajira Kwa Vijana

VETA Yaleta Mapinduzi ya Kilimo na Biashara Kupitia Bunifu –  Profesa Nombo

Makampuni 100 kushiriki maonesho ya OSHA Njombe

Malecela: Nitakuza Vipaji, Nitafutia Vijana Ajira Dodoma Mjini

Profesa Ndunguru: Tumewezesha Usafirishaji wa Mazao Mbalimbali Yenye Thamani ya Trilioni 15.6

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Bajeti Yadhihirisha Uhakika Wa Nishati Nchini
Next Article Program Ya Mama Samia Ya Kurasimisha Ujuzi Yazinduliwa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Program Ya Mama Samia Ya Kurasimisha Ujuzi Yazinduliwa
Habari April 23, 2026
Bajeti Yadhihirisha Uhakika Wa Nishati Nchini
Habari April 23, 2026
Ushirikiano wa TEA, Halmashauri wapewa msukumo kuimarisha mifuko ya elimu
Habari April 22, 2026
Kisima Kimoja Cha Gesi Chaonesha Mshangao Kwa Uzalishaji Wa Gesi-PURA
Habari April 22, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?