MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TAA Yasisitiza Uwajibikaji katika Utoaji wa Huduma
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TAA Yasisitiza Uwajibikaji katika Utoaji wa Huduma
Habari

TAA Yasisitiza Uwajibikaji katika Utoaji wa Huduma

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imeendelea kuimarisha utoaji wa huduma kwa kuzingatia uwajibikaji, uwazi na weledi, sambamba na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga kuboresha usafiri wa anga na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa TAA,  Irene Minja, wakati wa Maadhimisho na Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
Minja amesema kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu isemayo “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu” inaakisi dhamira ya TAA ya kuhakikisha wananchi na wadau wanapata huduma bora, salama na zenye ufanisi mkubwa.
Habari Picha 12592
Amefafanua kuwa TAA ni taasisi ya Serikali yenye jukumu la kujenga, kuendeleza, kusimamia na kuendesha viwanja vya ndege vya Serikali Tanzania Bara, na kwamba imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya sekta ya usafiri wa anga.
Kwa mujibu wa Minja, maboresho ya miundombinu ya viwanja vya ndege yana mchango mkubwa katika kukuza biashara, utalii na uwekezaji, huku yakirahisisha usafirishaji wa watu na mizigo ndani na nje ya nchi.
Amesema viwanja vya ndege vinaendelea kuwa lango muhimu la kuunganisha Tanzania na mataifa mbalimbali duniani, hivyo uwekezaji unaofanywa katika sekta hiyo unalenga kuimarisha ushindani wa nchi na kuvutia fursa zaidi za kiuchumi.
“Tunatambua mchango mkubwa wa viwanja vya ndege katika maendeleo ya taifa. Ndiyo maana tunaendelea kuboresha huduma na miundombinu ili kuhakikisha Tanzania inakuwa kivutio kikubwa cha watalii, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali duniani,” amesema.
Aidha, amewahimiza wananchi kutembelea banda la TAA katika maonesho hayo ili kupata taarifa sahihi kuhusu huduma zinazotolewa na mamlaka hiyo, kujifunza kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na kutoa maoni yatakayosaidia kuboresha zaidi utoaji wa huduma kwa umma.
Amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya wananchi na taasisi za umma ni muhimu katika kufanikisha utoaji wa huduma bora na maendeleo endelevu ya taifa.

You Might Also Like

Rais Mwinyi adhamiria kusimamia ubora wa bidhaa

Rais Samia akisikiliza jambo

Katibu Mkuu Ahimiza Uzalendo Na Uadilifu Kwa Wanachama wa Ewura CCC

Serikali Kushughulikia Utitiri Wa Vyama Ndani Ya Sekta Binafsi

Profesa Silayo Aaga, Jawara Kuchukua Uongozi Mpya wa AFWC25

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article ‎NIRC Imechimba Visima 362, , Yahamasiha Wakulima Kunufaika Na Program Ya Umwagiliaji
Next Article TMA Yatoa Elimu ya Hali ya Hewa kwa Wananchi Dodoma
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TMA Yatoa Elimu ya Hali ya Hewa kwa Wananchi Dodoma
Habari June 23, 2026
‎NIRC Imechimba Visima 362, , Yahamasiha Wakulima Kunufaika Na Program Ya Umwagiliaji
Habari June 23, 2026
Katibu Mkuu Uchukuzi Aipongeza TASAC,  Kuelimisha Wananchi 
Habari June 22, 2026
Qwaray Aipongeza VETA kwa Kukuza Ujuzi wa Vijana
Habari June 22, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?