MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali Kuimarisha Uvuvi Bahari Kuu Kupitia TAFICO
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali Kuimarisha Uvuvi Bahari Kuu Kupitia TAFICO
Habari

Serikali Kuimarisha Uvuvi Bahari Kuu Kupitia TAFICO

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Lyatuu,Dodoma
WAZIRI  wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, amesema Serikali inaendelea kuliimarisha Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)  kwa kulipatia vitendea kazi vya kisasa na kuendeleza miundombinu ya uvuvi ili kuongeza tija katika sekta hiyo na kukuza uchumi wa buluu nchini.
Akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo Bungeni mjini Dodoma leo, kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Dkt. Bashiru amesema Serikali, kupitia ufadhili wa Programu ya Maendeleo ya Uchumi na Jamii ya Japan, imepokea meli ya kisasa ya uvuvi wa bahari kuu, ambayo   ilizinduliwa rasmi Aprili 25, 2026 na RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema ujio wa meli hiyo ni hatua muhimu ya kuongeza uwezo wa Tanzania kuvuna rasilimali za uvuvi katika Ukanda Maalum wa Uchumi wa Bahari (EEZ), pamoja na kuongeza mchango wa sekta ya uvuvi katika pato la taifa na ajira.
Ameongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali imekamilisha ukarabati wa gati maalum la kushusha na kupandishia mazao ya uvuvi katika meli  lililopo Ras Mkwavi, ambalo sasa liko tayari kuhudumia shughuli za meli za uvuvi wa bahari kuu na kuongeza ufanisi wa shughuli za Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).
Amesema kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Serikali imepanga kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati katika sekta ya uvuvi, ikiwemo Kukamilisha ununuzi wa meli mbili za uvuvi wa bahari kuu, Kukamilisha usanifu wa kina na kuanza ujenzi wa Bandari ya Uvuvi ya Bagamoyo.
Miradi mingine ni Kuendelea kuimarisha ulinzi wa rasilimali za uvuvi, Kutafuta na kupanua masoko ya bidhaa za uvuvi ndani na nje ya nchi; Ujenzi wa miundombinu ya kuimarisha mnyororo wa thamani kwa mazao ya uvuvi.
Katika hatua nyingine amesema, Serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), ikiwemo ukarabati wa ghala la kuhifadhi samaki kwa ubaridi, kiwanda cha uchakataji wa mazao ya uvuvi pamoja na uzalishaji wa chakula cha samaki.
Amesema Serikali pia inaendelea kuongeza vifaa vya kisasa vya uchakataji na uhifadhi wa samaki ili kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi na kuvutia uwekezaji zaidi katika sekta ya uvuvi wa bahari kuu.
Aidha, Serikali inalenga kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi ya uvuvi wa kisasa, hatua inayokusudiwa kuhakikisha Tanzania inanufaika zaidi na rasilimali za Bahari Kuu. Ushirikiano huo ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050, ambayo inalenga kuongeza utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia ubia kati ya Serikali na sekta binafsi kwa asilimia 70.

You Might Also Like

Mapinduzi ya Elimu Geita: Wasichana Wamerudi Shule kwa Kasi

Tanzania Yaongeza Kasi ya Utafutaji Masoko ya Parachichi Ulaya

Thamani ya Fedha Ionekane Kwenye Utekelezaji wa Miradi-Nyamoga

Wakulima Wa Zabibu Wakiri Bidhaa Zilizoongezwa Thamani Zina Soko

MSD Yaokoa Zaidi Ya Mil. 15

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TPHPA Yaimarisha Mapambano Dhidi Ya Visumbufu Vya Mazao
Next Article TFS Yavunja Rekodi Utalii Wa Misitu,Mapato Yapaa Kwa Asilimia 43
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TFS Yavunja Rekodi Utalii Wa Misitu,Mapato Yapaa Kwa Asilimia 43
Habari May 15, 2026
TPHPA Yaimarisha Mapambano Dhidi Ya Visumbufu Vya Mazao
Habari May 14, 2026
Mbunge Ngorongoro Aiomba Serikali Kufungua Uchumi Loliondo
Habari May 13, 2026
TMA Yakamilisha Ufungaji Mitambo Ya Uangalizi Mpanda, Pemba
Habari May 13, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?