MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Dkt. William Ruto Aipongeza NSSF Tanzania Kwa Uwekezaji wa Dola zaidi ya Milioni 51 Nairobi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Dkt. William Ruto Aipongeza NSSF Tanzania Kwa Uwekezaji wa Dola zaidi ya Milioni 51 Nairobi
Habari

Dkt. William Ruto Aipongeza NSSF Tanzania Kwa Uwekezaji wa Dola zaidi ya Milioni 51 Nairobi

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
RAIS wa Kenya,  Dkt. William Ruto, ameusifu uwekezaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wa Tanzania unaoendelea jijini Nairobi, akisema ni mfano bora wa matumizi sahihi ya akiba za wanachama katika kukuza uchumi na maendeleo ya kikanda.
Habari Picha 11986
Akizungumza Mei 5, 2026 wakati akihutubia Bunge jijini Dodoma, Dkt. Ruto amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Tanzania,  Masha Mshomba, kwa usimamizi thabiti wa uwekezaji huo, akibainisha kuwa unaonesha namna bora ya kugeuza akiba za wanachama kuwa miradi yenye tija.
Amesema mradi huo uliopo eneo la Upper Hill, jijini Nairobi, unahusisha ujenzi wa majengo pacha yenye ghorofa 22, unaogharimu takribani dola za Marekani zaidi ya Milioni 51.
Mradi huo unatekelezwa kwa kutumia akiba za wanachama wa NSSF Tanzania na unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miaka miwili.
Dkt. Ruto ameeleza kuwa uwekezaji huo ni somo muhimu kwa Kenya na mataifa mengine ya Afrika Mashariki kuhusu umuhimu wa kukuza utamaduni wa akiba na uwekezaji kwa maendeleo ya muda mrefu.
“Uwekezaji ni zao la akiba. Huwezi kuwekeza kama huna akiba,” alisisitiza Dkt. Ruto, akihimiza wananchi na taasisi kuzingatia nidhamu ya kuchangia katika mifuko ya hifadhi ya jamii kwa mustakabali wa baadaye.
Aidha, amebainisha kuwa nchini Kenya wamefanya maboresho ya mfumo wa hifadhi ya jamii mwaka 2023 baada ya kujifunza kutoka mifumo bora ikiwemo ya Tanzania.
Ameeleza kuwa mfumo huo unahitaji mwajiri na mwajiriwa kuchangia kwa pamoja hadi asilimia 20 ya mapato ili kuimarisha usalama wa kifedha kwa wafanyakazi wanapostaafu.
Dkt. Ruto amesisitiza kuwa utamaduni wa kujiwekea akiba unapaswa kuendelezwa ndani ya jamii, akieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kujenga mifumo imara ya hifadhi ya jamii.
Rais Dkt. Ruto pia amesifu mafanikio ya Tanzania katika sekta ya hifadhi ya jamii, akieleza kuwa Kenya inaendelea kujifunza na kuchukua mifano bora kutoka kwa majirani zake.
Katika kuimarisha ushirikiano wa kikanda, amesema anajivunia uhusiano mzuri uliopo kati ya Kenya na Tanzania chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akibainisha kuwa huu ni wakati muhimu katika historia ya mataifa hayo mawili.
Akihitimisha, Dkt. Ruto amesema kuwa kwa sasa kuna hatua kubwa ya kihistoria katika uhusiano wa Kenya na Tanzania, akieleza furaha yake kwa ushirikiano wa karibu kati yake na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema viongozi hao wanafanya kazi kwa pamoja kuwaleta karibu wananchi wa Afrika Mashariki na kuondoa changamoto zilizodumaza maendeleo kwa muda mrefu.
Kauli hiyo inaakisi mwelekeo wa mataifa ya Afrika Mashariki katika kutumia rasilimali zao za ndani kama kichocheo cha ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.
Rais Dkt. William Ruto anahitimisha ziara rasmi ya siku mbili nchini Tanzania, iliyoanza Mei 4 hadi 5, 2026.

You Might Also Like

Maganga Atembelea Banda La Ofisi Ya Waziri Mkuu, Maonesho Ya Wiki Ya Vijana Mbeya

Manyara Kusambaza Mitungi 16,275 ya Gesi kwa Bei ya Ruzuku

Kadi za mpiga kura zenye jina la zamani la Tume ni halali

Majaliwa Aagiza Kuimarishwa kwa Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini

LATRA Yaboresha Mfumo Wa Taarifa Kwa Abiria

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ruto: Uwekezaji wa NSSF Nairobi ni mfano bora wa matumizi ya akiba
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Ruto: Uwekezaji wa NSSF Nairobi ni mfano bora wa matumizi ya akiba
Habari May 5, 2026
Waziri Aweso Aainisha Mikakati ya Kuboresha Huduma ya Maji
Uncategorized May 5, 2026
Wizara ya Maji Yawasilisha Vipaumbele 2026/2027 kwa Bajeti ya Trilioni 1.2
Habari May 5, 2026
CCM  Yapokea Mapendekezo Ya Tume Ya Kuchunguza Vurugu Za Uchaguzi Oktoba 25,2025
Habari May 5, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?