MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TPHPA Yaimarisha Mapambano Dhidi Ya Visumbufu Vya Mazao
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TPHPA Yaimarisha Mapambano Dhidi Ya Visumbufu Vya Mazao
Habari

TPHPA Yaimarisha Mapambano Dhidi Ya Visumbufu Vya Mazao

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Lucy Ngowi
DODOMA: SERIKALI imesema itaendelea kuimarisha utendaji wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) ili kuhakikisha sekta ya afya ya mimea inalindwa kwa ufanisi na kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao nchini.
Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde, alisema hayo jijini Dodoma wakati akimwakilisha Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Afya ya Mimea yaliyofanyika viwanja vya NaneNane Nzuguni.
Habari Picha 12046
Akizungumza katika maadhimisho hayo yenye kaulimbiu ya ‘Ulinzi wa Bayoanuai ya Mimea kwa Usalama wa Chakula na Lishe’, Silinde alisema afya ya mimea ni msingi muhimu wa usalama wa chakula, lishe bora, ajira na ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya kilimo.
Alisema Serikali inalenga kuimarisha ushirikiano wa taasisi mbalimbali katika kusimamia afya ya mimea, mazingira, wanyama na binadamu ili kukabiliana na changamoto za visumbufu vya mazao zinazoongezeka duniani.
“Changamoto za afya ya mimea haziwezi kutatuliwa na nchi au taasisi moja pekee, hivyo ushirikiano wa pamoja unahitajika ili kulinda uzalishaji wa mazao na mazingira,” alisema.
Habari Picha 12047
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Joseph Ndunguru, alisema mamlaka hiyo imefanikiwa kudhibiti visumbufu mbalimbali vya mazao nchini, hatua iliyochangia kuimarika kwa usalama wa chakula.
Alisema katika mwaka 2024/2025 Tanzania ilifikia utoshelevu wa chakula kwa asilimia 130 baada ya kuzalisha tani zaidi ya milioni 23 za mazao ya chakula.
Profesa Ndunguru alisema TPHPA imefanikiwa kudhibiti baa la panya katika mikoa 19, kudhibiti ndege waharibifu aina ya kwelea kwelea zaidi ya milioni 231, viwavijeshi katika hekta 219,411 pamoja na nzige waliovamia maeneo mbalimbali nchini.
Aidha alisema mamlaka hiyo imeendelea kufuatilia matumizi ya viuatilifu, kudhibiti magugu vamizi katika Ziwa Victoria na kufanya uchunguzi wa masalia ya viuatilifu kwenye mazao ya chakula ili kulinda afya za walaji na mazingira.
Habari Picha 12048

You Might Also Like

MBUNGE wa Kasulu Mjini Ahoji Serikali Kuhusu Mradi wa Maji Mwanga B

Profesa Ndunguru Abainisha Mwelekeo Mpya Wa Mageuzi Ya Kilimo Duniani

USAID yatoa Dola mil nane Kwa kampuni za Tanzania

Mgombea Udiwani Manyoni Adhalilishwa, Rushwa Yadaiwa Kuvuruga Kura Za Maoni

Mchengerwa Aongoza Ujumbe Wa Tanzania Kwenye Uzinduzi Wa Mkutano Wa Dunia Wa Tiba Asili

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mbunge Ngorongoro Aiomba Serikali Kufungua Uchumi Loliondo
Next Article Serikali Kuimarisha Uvuvi Bahari Kuu Kupitia TAFICO
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TFS Yavunja Rekodi Utalii Wa Misitu,Mapato Yapaa Kwa Asilimia 43
Habari May 15, 2026
Serikali Kuimarisha Uvuvi Bahari Kuu Kupitia TAFICO
Habari May 14, 2026
Mbunge Ngorongoro Aiomba Serikali Kufungua Uchumi Loliondo
Habari May 13, 2026
TMA Yakamilisha Ufungaji Mitambo Ya Uangalizi Mpanda, Pemba
Habari May 13, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?