MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TFS Yavunja Rekodi Utalii Wa Misitu,Mapato Yapaa Kwa Asilimia 43
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TFS Yavunja Rekodi Utalii Wa Misitu,Mapato Yapaa Kwa Asilimia 43
Habari

TFS Yavunja Rekodi Utalii Wa Misitu,Mapato Yapaa Kwa Asilimia 43

Author
By Author
Share
5 Min Read
Na  Lucy Lyatuu Dodoma
WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umeandika historia mpya katika sekta ya uhifadhi na utalii ikolojia baada ya kuongeza idadi ya watalii wa misitu hadi 329,753 na kukusanya zaidi ya Sh bilioni 3.09 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, hatua inayotafsiriwa kama mafanikio makubwa ya serikali katika kuigeuza misitu kuwa injini mpya ya uchumi wa utalii nchini.
Takwimu hizo zimetolewa   bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, wakati akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya Wizara  Ya Maliasili Na Utalii  kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Habari Picha 12057
Amesema  ongezeko hilo la watalii ni sawa na asilimia 20 ikilinganishwa na watalii 275,723 waliotembelea vivutio vya utalii ikolojia katika kipindi kama hicho mwaka uliopita, huku mapato yakiongezeka kwa asilimia 43 kutoka Sh bilioni 2.16 hadi kufikia Sh bilioni 3.09.
Amesema  mafanikio hayo yanatajwa kuchochewa na uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya utalii wa misitu, kampeni za matangazo na matukio ya michezo ya utalii yaliyoendelea kuvuta maelfu ya wageni wa ndani na nje ya nchi.
Habari Picha 12058
Katika mwaka uliopita pekee, TFS ilijenga malango sita ya kisasa katika maeneo ya Meru, Vikindu, Mwambesi, Pindiro, Mlima Rungwe na Ziwa Duluti; kujenga njia maalumu za watembea kwa miguu (board walks) katika misitu ya Sahare-Tanga na Amani; pamoja na kukarabati zaidi ya kilomita 287 za njia za watalii katika hifadhi 24 za misitu nchini.
“Mashindano na matamasha ya utalii yaliyofanyika ndani ya misitu yameendelea kuwa nyenzo mpya ya kutangaza vivutio vya Tanzania. Miongoni mwa matukio hayo ni pamoja na Tukutane Mt. Rungwe Season II, Meru Adventure Race, Mkwawa Rally, Rombo Marathon, Kalambo Waterfalls Utalii Festival na Uni Pugu Easter Experience,” amesema.
Amesema i na mafanikio ya utalii, serikali imeendelea kuonyesha makucha katika vita dhidi ya uharibifu wa misitu na biashara haramu ya mazao ya misitu.
Habari Picha 12059
Waziri Kijaji amesema TFS ilifanya doria za kimkakati 363 na doria za kawaida 12,854 katika hifadhi mbalimbali, hatua iliyosaidia kukamatwa kwa watuhumiwa 1,925 wa uhalifu wa misitu.
Amesema Kupitia operesheni hizo, serikali ilikamata na kutaifisha magunia 39,900 ya mkaa, mbao 31,046 zenye ujazo wa mita za ujazo 1,321, magogo 1,556 pamoja na mifugo zaidi ya 29,000 iliyokuwa ikiingizwa kwenye maeneo ya hifadhi kinyume cha sheria.
Katika hatua nyingine, TFS imeendelea kuimarisha vita dhidi ya moto wa misitu kwa kutumia teknolojia ya satelaiti kubaini matukio mapema, pamoja na kutoa mafunzo kwa vikosi 45 vya zimamoto na wananchi zaidi ya 20,000 wanaoishi jirani na hifadhi.
“Kutokana na juhudi hizo, matukio ya moto wa misitu yamepungua kwa wastani wa asilimia 11 kila mwaka, huku ukubwa wa maeneo yanayoteketea ukiendelea kupungua,” amesema.
Amesema Serikali  imeendelea kuwekeza kwenye upandaji miti na urejeshaji wa mazingira yaliyoharibiwa. Katika mwaka huu, TFS imeanzisha mashamba mapya ya miti ya Geita na Rwamgasa yenye ukubwa wa hekta 28,000, sambamba na kuzalisha miche milioni 32.8 ya miti iliyogawiwa kwa wananchi na taasisi mbalimbali kwa ajili ya upandaji.
Kuhusu mikoko, amesema zaidi ya miche milioni 37.2 imepandwa katika mikoa ya Tanga na Pwani kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, hatua inayolenga kuimarisha uhifadhi wa mwambao wa Bahari ya Hindi dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.
Habari Picha 12060
Amesema Sekta ya nyuki nayo imeendelea kuonyesha matumaini makubwa kiuchumi baada ya Tanzania kufanikiwa kuuza tani 1,076.8 za asali zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 12.9 katika masoko ya Ulaya na Marekani.
Waziri Kijaji amesema mafanikio hayo yamekuja baada ya sampuli 132 za asali kutoka wilaya 31 kupimwa katika maabara ya kimataifa nchini Ujerumani na kuthibitishwa kukidhi viwango vya ubora wa kimataifa.
“Matokeo yanaonyesha asali ya Tanzania ni bora na inakidhi vigezo vya kuuzwa katika masoko ya ndani na nje ya nchi,” amesema.
Habari Picha 12061

You Might Also Like

MOI Yaeleza Sababu Viungo Bandia Kuuzwa Kwa Bei Kubwa

Mnyororo wa Biashara Kariakoo Unafanywa Na Wageni

Aprili 2025 Matokeo Awamu Ya Kwanza, Maoni Dira Ya Taifa Na Maendeleo 2050 Kutolewa

TOSCI: Mbegu Bora Ni Ajira, Biashara

JAB Yasisitiza Ithibati Kama Njia ya Kuimarisha Ubora na Uaminifu wa Habari

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Kuimarisha Uvuvi Bahari Kuu Kupitia TAFICO
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Serikali Kuimarisha Uvuvi Bahari Kuu Kupitia TAFICO
Habari May 14, 2026
TPHPA Yaimarisha Mapambano Dhidi Ya Visumbufu Vya Mazao
Habari May 14, 2026
Mbunge Ngorongoro Aiomba Serikali Kufungua Uchumi Loliondo
Habari May 13, 2026
TMA Yakamilisha Ufungaji Mitambo Ya Uangalizi Mpanda, Pemba
Habari May 13, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?