Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa William Anangisye amewataka wahitimu chuoni hapo kulinda tunu za taifa ambazo ni amani, umoja, uhuru, Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar.
Profesa Anangisye ametoa rai hiyo wakati wa Mahafali ya 55 Duru ya Kwanza yaliyofanyika Mlimani City, Dar es Salaam.
“Lindeni tunu ya Taifa. Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna taifa au nchi nyingine ambayo wewe na mimi tunaweza kuita nyumbani isipokuwa Tanzania.
“Hivyo popote mtakapokuwa na nitakapokuwa, tunao wajibu mkubwa wa kulinda tunu za taifa,” amesema.
Pia amewaasa wahitimu kutambua thamani ya elimu waliyoioata kwa kuwa imewaongezea thamani kwani wana nafasi ya kipekee kuwa mawakala wa mabadiliko.
Kwa upande mwingine, amewataka wananchi kushiriki uchaguzi mkuu kwa kuwa ni haki ya kila mtanzania.
“Kwa mantiki hii, na kwa heshima kubwa niombe kila mmoja wetu, kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kuoiga kura,” amesema.
Naye Mwenyekiti wa chuo hicho, Balozi Mwanaidi Maajar amesena katika kuhakikisha chuo kinabaki kuwa kinara wa elimu, utafiti na uvumbuzi katika ukanda wa bara la Afrika, baraza linaendelea kusimamia miradi mikubwa ya naendeleo.