Nenda moja kwa moja kwenye maudhui
November 7, 2026
Habari Lucy Ngowi 5

WDC Kuboresha Miradi Yake Ya Majengo

Na Lucy Lyatuu
SHIRIKA la Maendeleo la  Wafanyakazi (WDC) lina mpango mkubwa wa maboresho ya miradi yake ya majengo nchini lengo likiwa ni kuongeza kipato  na kuongeza Fursa za biashara.
Meneja Mkuu wa WDC, Muchunguzi Kabonaki amesema hayo Dar es Salaam wakati akizungumza na gazeti la MFANYAKAZI kuelezea miradi inayosimamiwa na Shirika hilo  na mipango waliyonayo kwa ajili ya mabotesho.
Amesema WDC inajivunia kumiliki majengo mbalimbali nchini ikiwa ni uwekezaji wa wanachama kupata fedha badala ya malimbikizo ya michango.
Ameitaja mikoa ambayo Shirika limeweka vitega uchumi vyake ambavyo ni majengo kuwa ni pamoja na Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Moshi.
“Ikumbukwe kuwa WDC ni mwendeshaji wa baadhi ya vitega uchumi vya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi na Kwa Sasa linaendesha vitega uchumi vya makazi,” amesema.
Je, habari hii ilikusaidia?
Sambaza

Maoni 0

Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kutoa maoni!

Acha maoni

Barua pepe yako haitachapishwa. Sehemu zenye * ni lazima.