Na Lucy Lyatuu, DODOMA
WAKATi bunge likijadili bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mbunge wa viti Maalum Zuwena Bushiri amesema vijiji vinavyozunguka mlima Kilimanjaro havijawahi kupata fedha za uwajibikaji kwa jamii kwa miaka mitano licha ya kushiriki katika kulinda mazingira.
Amesema hayo jijini Dodoma wakati wabunge wakichangia, mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii bungenni ambapo pia walitaka hatua za haraka zichukuliwe kudhibiti wanyama waharibifu na kuhakikisha wananchi wanaopata madhara wanalipwa fidia kwa wakati ili kuondoa migogoro kati ya wananchi na maeneo ya hifadhi.
Akizungumza Zuwena amesema wananchi wa vijiji hivyo wanatakiwa kupata fedha hizo hilo ,ili waendelee na shughuli zao za maendeleo pamoja na ulinzi wa mazingira ya mlima huo.
Ameongeza kuwa ipo haja ya Serikali kufanya tafiti za kina kuhusu kupungua kwa theluji ya Mlima Kilimanjaro akisema hali hiyo inaweza kuathiri utambulisho wa Tanzania kimataifa.
“Kwa sasa barafu inapungua kila siku ukilinganisha na miaka iliyopita. Serikali ifanye tafiti na ilete majibu ya namna ya kuokoa theluji hiyo,” amesema.
Kadhalika ametaka kuongezwa utangazaji wa vivutio vya utalii vilivyoko mkoa huo ikiwemo pango wanaloishi ngombe na mbuzi wasiokuwa na mmiliki katika mlima Kidenge.
Amesema wanyama hao wanaoishi katika pango hilo hujitenga wzkTi wa kulala kwa maana ya wakubwa na watoto la,ini pia asubuhi huanza ,utoka kwa kuzingatia u,ubwa,jambo ambalimlimekuwa likiwafurahisha watalii wanaofika katika mlima huo.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Christina Mzava, amesema sekta ya utalii ni ya pili kwa kuingiza mapato kwenye pato la taifai, na mapato ya sekta hiyo yameongezeka kutoka Sh bilioni 3.9 hadi Sh. bilioni 4.4 kufikia Desemba 2025.
Hata hivyo, amesema fedha hizo zinaingia kwenye mfuko mkuu wa Serikali lakini zinazorudishwa kwenye taasisi za utalii ni kiasi kidogo kisichotosheleza mahitaji ya sekta hiyo.
“Sekta hii ina mambo mengi ya kufanya ikiwemo kulinda wanyama, kuboresha vivutio na miundombinu ya utalii. Fedha hizi zingebaki kwao ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi,” amesema.
Kuhusu malalamiko ya wananchi wanaoathiriwa na wanyama wakali, alisema fidia zinazotolewa ni ndogo na hazitolewi kwa wkati licha ya madhara makubwa yanayowapata wananchi.
Amesema takwimu zinaonyesha madai ya fidia kwa wananchi walioathirika yanafikia dola 62,446 sawa na zaidi ya Sh bilioni 18.6 lakini hadi sasa ni dola 15,000 pekee zimelipwa huku zaidi ya Sh 47,000 zikidaiwa kwa zaidi ya miaka miwili.
Mbunge wa Pangawe, Haji Amour Haji, ameshauri mambo mbalimbali kwa Wizara ya Maliasili na Utalii ili kuvutiawatalii, ikiwemo suala la kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia slogan moja ya kudumu ya utalii pamoja na kuwatumia wahamasishaji maarufu duniani kuitangaza.
Amesema Tanzania imekuwa ikibadilisha ‘slogan’ za utalii mara kwa mara jambo linalopunguza nguvu ya utambulisho wake katika soko la kimataifa.
Aidha, Haji alisema utalii hauwezi kukua bila miundombinu bora, usalama wa uhakika, huduma nzuri za malazi pamoja na huduma bora kwa wateja.

