MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Ukosefu wa Chakula Shuleni Waathiri Wanafunzi Longido, CORDS Waja na Mrad
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Ukosefu wa Chakula Shuleni Waathiri Wanafunzi Longido, CORDS Waja na Mrad
Habari

Ukosefu wa Chakula Shuleni Waathiri Wanafunzi Longido, CORDS Waja na Mrad

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu, Longido
WANAFUNZI wa shule za msingi katika Wilaya ya Longido mkoani Arusha, wakiwemo wanafunzi wa Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Waliokosa (MEMKWA), wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa chakula shuleni hali inayotajwa kuathiri maendeleo yao ya kitaaluma.
Changamoto hiyo imebainishwa katika kikao cha Jukwaa la Wadau wa Elimu wilayani humo kilichoandaliwa na Shirika la Utafiti, Maendeleo na Huduma za Jamii (CORDS), kikihusisha viongozi wa halmashauri, waratibu elimu, viongozi wa vijiji, walimu pamoja na asasi za kiraia.
Akizungumza katika kikao hicho, Ofisa Elimu wa Kata ya Ngarenaibo, Paulo Teveli amesema baadhi ya wazazi hawapeleki chakula shuleni jambo linalochangia wanafunzi kushindwa kufanya vizuri darasani.
Amesema tatizo hilo linachangiwa na baadhi ya wazazi kutothamini elimu huku wengine wakikabiliwa na hali ngumu ya maisha.
Habari Picha 12079
“Tatizo hili linaathiri hata wanafunzi wa MEMKWA ambao katika kata yangu wako 31.
“Tunahitaji ushirikiano wa wadau wote kulitatua, huku tukithamini msaada tunaoupata kutoka CORDS katika sekta ya elimu,” amesema Teveli.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Longido, Sein Kitomali amesema wanafunzi wengi hutembea umbali mrefu kufika shule hivyo wanahitaji chakula na vifaa muhimu vya kujifunzia ili waweze kuzingatia masomo yao.
Amesema shule hiyo ina wanafunzi 62 wa MEMKWA, ambapo 38 wanatarajiwa kufanya mtihani wa darasa la nne mwaka huu.
Habari Picha 12080
Amebainisha kuwa msaada wa CORDS umechangia kuboresha mazingira ya kujifunzia kupitia utoaji wa vifaa mbalimbali vya shule.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngoswaki, Karia Mollel amesema jamii za wafugaji bado zina changamoto ya kuthamini elimu, lakini juhudi zinaendelea kuhamasisha wazazi kuwapeleka watoto shule na kuzuia ndoa za utotoni.
Meneja Elimu wa CORDS, Ezekiel Piniel amesema shirika hilo linaendesha Mradi wa Kupambana na Umasikini kupitia Elimu na Uwezeshaji wa Kiuchumi (BELIEF), unaofadhiliwa na Shirika la Stromme Foundation.
Amesema kupitia mradi huo, shule za Ngoswaki na Longido zinapatiwa vifaa vya kujifunzia, kuboreshwa miundombinu pamoja na kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Aidha, vijana na vikundi vya wajasiriamali vinawezeshwa kupitia mafunzo ya stadi za maisha na usimamizi wa miradi.
Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Longido, Nestory Dagharo amesema wazazi wanapaswa kuchangia chakula shuleni kwa kuwa ni sehemu ya wajibu wao katika kuhakikisha watoto wanapata elimu bora.

You Might Also Like

Wananchi Waendelee Kupewe Elimu Kuhusu Bioteknolojia

Makalla aitaka Halmashauri Longido kutenga fedha, ujenzi wa uzio Samia Girls

Ridhiwani Aongoza Majadiliano Ya Taarifa Ya Utekelezaji Wa Majukumu PSSSF

Maganga Atembelea Banda La Ofisi Ya Waziri Mkuu, Maonesho Ya Wiki Ya Vijana Mbeya

Mazao Ya Mikunde Yatajwa Kuwa Na Kiwango Kikubwa Cha Protini

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Waziri Kijaji: Huduma ya Kudungwa na Nyuki Kuongeza Kinga Yavutia Bungeni
Next Article Mbunge Ataka Vijiji Vinavyozunguka Mlima Kilimanjaro Kulipwa Fedha Za Uwajibikaji
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Uwekezaji wa Vijana Watajwa Chachu ya Ukuaji wa Uchumi
Habari June 29, 2026
Tanzania Yaendelea Kuimarisha Usalama Na Ulinzi Wa Taarifa Binafsi
Habari June 29, 2026
WCF Yapigia Debe Ushirikiano na Teknolojia Kuimarisha Hifadhi ya Jamii
Habari June 28, 2026
Sabasaba 2026 Kuingiza Teknolojia Mpya na Fursa za Uwekezaji
Habari June 27, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?