MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kanisa Laitaka Serikali Kuchukua Hatua Dhidi ya Rushwa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kanisa Laitaka Serikali Kuchukua Hatua Dhidi ya Rushwa
Habari

Kanisa Laitaka Serikali Kuchukua Hatua Dhidi ya Rushwa

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
DODOMA: ASKOFU wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Central Tanganyika, Dkt. Dickson Chilongani, ameitoa wito kwa Serikali kushughulikia kero mbalimbali zinazowakabili Watanzania ili kudumisha amani, haki na ustawi wa jamii.
Akizungumza leo jijini Dodoma wakati wa ibada ya maadhimisho ya sikukuu ya kumbukizi ya kufufuka kwa Yesu Kristo, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu, Dkt. Chilongani amesema kuwa hatua zaidi zinahitajika ili kutatua changamoto zinazowakwamisha wananchi katika maisha yao ya kila siku.
Amesema kuwa, licha ya juhudi zilizofanywa na Serikali ikiwemo kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma mwaka jana, bado kuna matatizo mengi yanayohitaji kushughulikiwa, hususan katika utoaji wa huduma serikalini.
“Tunashukuru kwa jitihada zilizofanyika, lakini bado kuna kero nyingi katika ofisi mbalimbali ambazo zinapaswa kupatiwa ufumbuzi wa haraka,” amesema.
Askofu Chilongani ametaja baadhi ya kero hizo kuwa ni pamoja na urasimu usio wa lazima, vitendo vya kunyimwa haki na ongezeko la rushwa, ambavyo vinaathiri utoaji wa huduma na haki kwa wananchi.
Ameongeza kuwa baadhi ya watumishi wamekuwa wakidai kile kinachoitwa ‘uwezeshwaji’, hali ambayo kimsingi ni rushwa, na kwamba vitendo hivyo vinafanyika waziwazi bila aibu.
“Unapotuma mtu kufuatilia jambo muhimu, anakwambia anaombwa ‘facilitation’. Hili ni tatizo kubwa, na wakati mwingine hata taasisi za dini zinaombwa kutoa fedha hizo. Serikali inapaswa kuingilia kati hali hii,” amesisitiza.
Katika kuhitimisha mahubiri yake, Dkt. Chilongani ameipongeza nchi kwa kuendelea kuwa na amani, umoja na mshikamano, akisisitiza umuhimu wa kuilinda misingi hiyo.
Amefananisha hali hiyo na simulizi ya wanawake waliokwenda kaburini kwa Yesu, ambapo waliondolewa hofu na changamoto zao na kubadilishiwa furaha, akieleza kuwa ni wajibu wa Serikali kuhakikisha Watanzania wanaishi kwa furaha kwa kuondoa kero zinazowakabili.

You Might Also Like

Mgahawa unaotembea fursa kwa vijana, kutoa huduma ya unywaji wa kahawa

TARURA Wataka Makandarasi Kulinda Njia Mbadala Kipindi cha Mvua Kubwa

Sheria  300 Zimetafsiriwa Kwa Lugha Ya Kiswahili

Rais Dk Mwinyi Kukata Keki Sabasaba

Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Wajitosa Kugombea Ubunge

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article CWT Yashauri Walimu Wasiwe Wasimamizi Wa Miradi
Next Article Kasekenya: Barabara ya Kakonko–Muhanga Ipo Katika Hatua za Awali za Kujengwa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

OUT: Elimu Sasa Kiganjani
Habari Uncategorized August 24, 2026
NGARUMA VTC  Kutoa Mafunzo Katika Fani Mbalimbali Za Ufundi
Habari August 24, 2026
VETA kumpa nafasi Igobeko kuongeza ujuzi na kuwawezesha wengine
Habari August 23, 2026
Airtel Yajenga Darasa La Fursa Katika Shule Ya Sekondari Magaoni,Tanga
Habari August 23, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?