Na Lucy Lyatuu
CHUO cha Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi NGARUMA VTC, kilichopo Marangu, Moshi Kilimanjaro ambacho kinasimamiwa na Kanisa la Kiinjili La Kilutheri Tanzania ( KKKT,) kimeeleza kutoa mafunzo katika fani mbalimbali zenye kutoa mwanga na ujuzi kwa mwanafunzi.
Fani zinazotolewa chuoni hapo nimpamoja na Ushonaji, Useremala, Ujenzi, Umeme, TEHAMA (ICT) na Ufundi wa Magari (Mechanics), yakitolewa na walimu wenye utaalamu na uzoefu katika fani hizo.



Mkuu wa Chuo hicho Beneth Mugyabuso, ametoa wito kwa vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini wenye nia ya kujifunza na kujenga maisha kupitia ujuzi wa ufundi kuchangamkia fursa hiyo na kujiunga na NGARUMA VTC
Amesema Chuo pia kimetangaza nafasi za mafunzo ya ufundi kwa wahitimu wa shule za msingi, sekondari na vyuo na zaidi kinatoa huduma kwa watoto wenye mahitaji.
Amesema NGARUMA VTC inatoa kozi za muda mfupi kwa ada nafuu, huku ikiwa imesajiliwa na NACTVET na kuwa na huduma za malazi kwa wanafunzi wa kike na wa kiume.



Amesema Kwa kuzingatia vijana kutoka mazingira yenye changamoto, chuo pia kina utaratibu wa kuwasaidia baadhi ya vijana kutoka familia zenye uhitaji na waliotelekezwa na wazazi kupata fursa ya ufadhili wa mafunzo ya ufundi, ili kuwawezesha kujenga ujuzi na maisha bora ya baadaye.


