MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kasekenya: Barabara ya Kakonko–Muhanga Ipo Katika Hatua za Awali za Kujengwa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kasekenya: Barabara ya Kakonko–Muhanga Ipo Katika Hatua za Awali za Kujengwa
Habari

Kasekenya: Barabara ya Kakonko–Muhanga Ipo Katika Hatua za Awali za Kujengwa

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
1 Min Read
Na Mwandishi Wetu
DODOMA: SERIKALI imetangaza mpango wa kujenga barabara ya Kakonko–Muhanga kupitia Gwarama yenye urefu wa kilomita 41.43 kwa kiwango cha lami, hatua inayolenga kurahisisha usafiri na usafirishaji kwa wananchi na wafanyabiashara.
Hayo yamebainishwa leo Aprili 8, 2026, Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi, Godfrey Kasekenya, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kakonko, Alan Mvano (CCM), aliyetaka kufahamu ni lini barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami.
Kasekenya amesema barabara hiyo ni barabara kuu inayosimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Kigoma, na kwa sasa Serikali ipo katika hatua za awali za kuandaa upembuzi yakinifu pamoja na usanifu wa kina.
Hii ni hatua muhimu kabla ya kuanza ujenzi rasmi wa lami.
Aidha, ameongeza kuwa mara usanifu utakapokamilika na gharama halisi za ujenzi zikajulikana, Serikali itahakikisha fedha za utekelezaji zinapatikana ili kuanza ujenzi.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kasekenya amemuagiza Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kigoma kuhakikisha barabara hiyo inakaguliwa na kufanyiwa matengenezo ya muda ili iweze kupitika kikamilifu, hivyo wananchi kupata huduma bora za usafiri na usafirishaji wakati ikisubiri ujenzi wa lami.

You Might Also Like

TEEA YAOMBA USHIRIKIANO NA WIZARA YA MADINI KUIMARISHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Yonaz akabidhi boti ya doria kukabili vitendo vya kiuhalifu

Mgombea Urais SAU Aahidi Kuongoza Nchi Kwa Hofu Ya Mungu

Kikosi Kazi Maalumu Cha Kupitia Muongozo Wa Ufasili Wa Sheria Chazinduliwa

Pinda Aitaka Jamii Kujikita Upandaji Miti Bila Kusubiri Matukio Maalumu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kanisa Laitaka Serikali Kuchukua Hatua Dhidi ya Rushwa
Next Article Mbunge Aibana Serikali Kuhusu Malipo ya Wafanyakazi wa Zamani SPM Mgololo
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

OUT: Elimu Sasa Kiganjani
Habari Uncategorized August 24, 2026
NGARUMA VTC  Kutoa Mafunzo Katika Fani Mbalimbali Za Ufundi
Habari August 24, 2026
VETA kumpa nafasi Igobeko kuongeza ujuzi na kuwawezesha wengine
Habari August 23, 2026
Airtel Yajenga Darasa La Fursa Katika Shule Ya Sekondari Magaoni,Tanga
Habari August 23, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?