Na Lucy Lyatuu,Tanga
MKUU Wa Idara Ya Mawasiliano Na Uhusiano Airtel,Jackson Mmbando amesema,watajenga darasa la fursa (smart class) katika shule ya sekondari Magaoni iliyoko jijini Tanga kwa lengo la kuwezesha wabunifu kupanua wigo wa mawazo yao.
Amesema hayo katika uzinduzi wa Program inayowezesha wabunifu kulinda na kumiliki mawazo yao na teknolojia zao ijulikanayo kama Inno IP pamoja na program ya Fursa Women Business ya kuwezesha wanawake kutumia mifumo ya kidigitali.


Mmbando amesema hayo katika katika hafla ya kutia saini ujenzi aa jengo hilo kwenye maadhimisho ya wiki ya Elimu,Ujuzi na Ubunifu 2026 inayoendelea katika viwanja vya Usagara jijini Tanga.
Program hizo zinatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Tume Ya Taifa Ya Sayansi Na Teknolojia (COSTECH) kupitia DTBi pamoja na Wakala Wa Usajili Wa Biashara Na Leseni (BRELA) pamoja na Airtel.
Kuhusu Airtel amesema kupitia Airtel Smart Class watatoa mafunzo ya ujasiriamali na kidijitali kwa wanawake na vijana.

Darasa kama hilo litakuwepo Magaoni na Usagara na kuwataka wabunifu na wajasiriamali kulitumia kukuza ujuzi.
“Tayari kuna darasa kama hilo katika shule mbalimbali nchini zikiendelea kuibua na kukuza vipaji vya vijana na wanafunzi katika ubunifu ikiwemo shule ya sekondari Kijitonyama Dar es Salaam,” amesema.




