Na Lucy Lyatuu, Dodoma
BODI ya Usajili Wa Wabunifu Majengo Na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) imesema ina kesi 300 mahakaman zinazohusu watu na kampuni zilizokiuka taratibu za ujenzi wa majengo mbalimbali kwa kutoshirikisha wataalam husika.
Kaimu Msajili wa Bodi hiyo,Daniel Matondo amesema hayo wakati akizungumza katika wiki ya utumishi wa umma inayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park mkoani Dodoma.
Amesema kesi hizo ziko maeneo mbalimbali nchini kama Mbeya, Arusha, Dodomam na kwamba Dar es Saalm inaongoza kwa mashauri mengi.

Amesema wanashiriki katika maonesho hayo kutoa elimu mbalimbali na kutoa tahadhari kwa wananchi kuwa wasijenga bila kushirikisha wataalam wa bodi hiyo na kwamba wanapokwenda kinyume sheria huchukua mkondo wake.
“Yapo majengo ya aina mbalimbali yaliyoguswa kwenye sheria kwamba yale ya ghorofa lazima yahusishe wataalam wa bodi katika kubuni na kusimamia,”amesema na kuongeza kuwa majengo yote ya umma kama mashule,hospitali na viwanja vya mpira,maghala na majengo ya viwanda.
Amesema licha ya kwamba wananchi wameanzamkupata elimu wengi wakipewa vibao vya ujenzi bado wako wachache wanaopata shida lakini bodi inaendelea kuwaelimisha na wanaokaidi hupelekwa mahakamani ama kutozwa faini.

Matondo amewataka wananchi kutosubiri hadi kupelekwa Mahakamani bali ni muhimu kujisajili kwa hao watalam na kupata huduma kama inavyostahili.
Hata hivyo alisema kwa anayetuhumiwa hupewa notisi ya kwanza hadimya tatu na asiposikia ndipo hupelekwa mahakamni ili hakimiweze kutendeka.
Kuhusu wikinya utumishi amesema wanaitumia kutoa elimu kuhusu huduma wanazotoa za wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi na kwamba wananchi watumie fursa hiyo kupata elimu na kuepuka madhara.

Alisema pia bodi hutoa mafunzo kwa wataalam wao kwa ajilimya kuwaongezea ujuzi na kwamba hufanya mitihani kwa wanaomaliza vyuo vikuu ili kuendeleza taaluma hiyo.
hivyo alisema kwa anayetuhumiwa hupewa notisi ya kwanza hadimya tatu na asiposikia ndipo hupelekwa mahakamni ili hakimiweze kutendeka.
Kuhusu wikinya utumishi amesema wanaitumia kutoa elimu kuhusu huduma wanazotoa za wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi na kwamba wananchi watumie fursa hiyo kupata elimu na kuepuka madhara.
Alisema pia bodi hutoa mafunzo kwa wataalam wao kwa ajilimya kuwaongezea ujuzi na kwamba hufanya mitihani kwa wanaomaliza vyuo vikuu ili kuendeleza taaluma hiyo.


